IJUE ETHIOPIA NCHI AMBAYO HAIJAWAHI TAWALIWA

MACHACHE YAHUSUYO 'NCHI YA WAHABESHI'
Ethiopia -Neno la Kigiriki likimaanisha Ngozi iliyoungua/Burnt Face ama ngozi nyeusi (Mwafrika)
1. Nchi Pekee ambayo KAMWE haijalivaa kongwa la MKOLONI...Ethiopia Imeitwanga Italia Mara Mbili Ikijinasua na Ukoloni............Ethiopia ni nchi ya 10 kwa ukubwa Afrika na hadi mwaka 2008 ilikua na watu milioni 82 na upasta/ushee (takribani mara mbili ya Tanzania kwa sensa ya 2012 .......Ni vyema utambue pia kwamba Hili ni moja ya Mataifa Makongwe Duniani (since 980 BC)
2. Mmea wa Kahawa uligunduliwa na Wachunga Mbuzi Baada ya Kumuona Mbuzi akipepesuka mara baada ya kukatiza mashamba ya Kahawa
3. Muhabeshi Abebe Abikula Ndiye Mwafrika wa Kwanza Kutwaa Medali ya Dhahabu kwenye Mashindano ya Olimpiki mnamo mwaka 1960 huku akiwa amevalia VIATU VYA KULALIA (PEKU/Bare foot) Wafukuza upepo wengine maarufu ni Tirunesh Dibaba na Haile Gebrselassie. Riadha ndiyo mchezo ambao umeipaisha Ethiopia kwenye duru za Kimataifa
3. Nchi Pekee Duniani yenye Miezi 13 Badala ya 12 Iliyozoeleka ...kwa mantiki hiyo Ethiopia ama 'Uhabeshi' kwa kiswahili iko nyuma Miaka 8 kwa Kalenda ya Mzungu (Western Calendar)........Septemba 11 ndiyo SIKUKUU YA MWAKA MPYA Ethiopia  ...ukifika Ethiopia leo mwaka unasomeka 2009
4. Mfalme Menelik II ndiye Mwafrika wa Kwanza KUENDESHA GARI ambalo lilifika Ethiopia Mnamo 1907 punde tu baada ya Vita ya Majimaji huku Bongo
5. Waethiopia wengi hujinasibu kwamba wao ni wa mbari ya Mfalme Suleiman na Malikia wa Sheba ..........
6. Ethiopia Inatajwa mara AROBAINI katika Msahafu wa Bibilia. Ethiopia ni moja ya Nchi chache ambazo zimetajwa na Misahafu yote miwili ya DINI KUU yaani Bibilia na Quran Tukufu, kadhalika kwenye magombo mengi ya kale............
7.  Ethiopia ndilo chimbuko la Umajumui wa Afrika (Pan-African ism) chini ya Mfalme Haile Selasie na Kuchagiza Kuzaliwa kwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU)
8. Miongoni mwa mbari ya Mursi huko Kusini ya Ethiopia, Msichana mwenye mdomo ulionakshiwa kwa kisahani (Disc) ndiye huonekana mlimbwende miongoni mwa wengi
9. Ethiopia ndilo chimbuko/source? la Mto Nile na yasemekana pia una asili ya muunganiko na Bustani ya Edeni (naendelea kuchimba)....Mto Nile ndio mrefu zaidi duniani
10. Mji Mkuu wa Ethiopia (Nakusudia Addis Ababa Ikimaanisha Maua Mapya/'New Flower') uko mwinuko wa Mita 2,400 na ndio  ndilo Jiji la Tatu kwa kwa kujenga juu zaidi ya mwinuko juu ya usawa wa Bahari Duniani....zaidi ya 70% ya Milima yote Afrika Hupatikana Ethiopia
11. Kama ambavyo HUENDA ni utovu wa nidhamu kutomuamkia mtu aliyekuzidi makamo huku Tz, ni UTOVU MKUBWA WA NIDHAMU KUKATAA KUKIRIMIWA KAHAWA ..................unavyomkaraibisha mgeni soda hapa wao ni mwendo wa KAHAWA ..........
12. Licha ya kuwa mzalishaji mkuu wa Kahawa Duniani (5th), Ethiopia ni Nchi ya TANO kwa Ufukara Afrika, zaidi ya 66% wanaishi chini ya DOLA 1 KWA SIKU (Buku mbili kuanzia chai hadi dinner) na ndiyo nchi ambayo lishe DUNI imefanya wstani wa kuishi uwe mdogo zaidi kuliko nch zote (Miaka 50 wanawake na 48 wanaume)
13. Uwe makini kuhesabu masaa uwapo Ethiopia (In Ethiopia, time is counted differently. Six o’clock is said to be 12 o’clock, and 16:00 hours is 10 o’clock. Ethiopians rationalize that the clock should start when the day does.)
14. Ukiacha Waarabu, Wahabeshi ndilo Taifa pekee linalotumia silabi zake yenyewe (except for the Arabs, the Ethiopians are the only people in Africa with their own indigenous written alphabet)
15 Baadhi ya Rangi za Bender za Mataifa ya Afrika zimeakisi/kushabihiana na Ethiopia sababu ndiyo nchi ya kwanza kuishinda dola/Nguvu ya Kijeshi ya Mzungu (Kichapo cha Italia) Baadhi ya nchi hizo ni PAMOJA NA GHANA ambayo ndiyo ya kwanza kujipatia Uhuru wake (Tizama Bendera ya Ghana na ya Ethiopia)
16. WAHABESHI husalimiana kwa kushikana mikono na kugonganisha mabega ikiashiria Ukamanda/salam ya Ungangari
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA

ZAKIA MEGHJI AWATIA HAMASA GIRL GUIDES, ATAKA WAWE JASIRI

DC MKURANGA AZINDUA MRADI WA MASHAMBA MJI YA NAMAINGO MSOLWA

TGGA WAMUAGA BOSS WA GIRL GUIDES AFRIKA KWA HAFLA KABAMBE

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

Wasafi TV kuanza kurusha matangazo yake leo (+video)