IJUE NDEGE YA RAIS WA MAREKANI(AIR FORCE ONE) KWA UNDANI


• Ina kitanda, bafu, gym na ofisi ya rais
• Inaweza kujijaza mafuta yenyewe ikiwa angani
• Inahifadhi aina 2000 za vyakula
• Ina hospitali na duka kubwa la dawa baridi
• Ina internet na simu zinazoweza kuwasiliana na watu ikiwa angani
• Injini zake nne zina mhimili(thrust) pauni 56,700( zinaweza kuisaidia Tanesco kufua umeme zaidi ya megawatt 200
Na Kizito Makoye pamoja na mtandao
Nikiwa safarini nchini Marekani kwa mara ya kwanza mwaka 2007, chini ya programu ya waandishi wa habari za uchunguzi ijulikanayo kama International Visitors Leadership Programme, inayofadhiliwa na wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo, nilipata fursa ya kutembelea makao makuu ya wizara ya ulinzi ya nchi hiyo Pentagon pamoja na ngome ya kijeshi ya nchi hiyo yenye uwanja mkubwa wa ndege Andrews Airbase Jijini Washington, ambapo ndipo ndege kubwa ya Rais wa nchi hiyo Donald Trump huegeshwa. Ngoja kidogo niwaeleze maajabu ya ndege hiyo
Air Force one ni alama kuu ya nchi ya Marekani na hasa ofisi ya Rais. Kila mara Rais anaposafiri kwenda ng'ambo au safari za ndani , huitumia ndege hiyo ya kisasa aina ya Jumbo Jet. Tarehe 11 September , ndege hiyo ilithibitisha kuwa ni zaidi ya chombo cha usafiri--iligeuka kuwa handaki la angani wakati ambapo ardhi ya marekani haikuwa salama tena kufuatia mashambulizi ya kigaidi. Kwenye makala hii tutajifunza namna Air Force One inavyofanya kazi wakati Rais wa taifa hilo kubwa lenye watu zaidi ya million 300 ikimsafirisha Donald Trump. Katika kila kitu ambacho Airforce One inabeba, haishangazi kusikia vyombo vya habari vikiita ni " Nyumba Nyeupe inayoruka"( Flying White House)
Watu wengi wana wazo la ujumla kwamba ndege ya Rais ni ofisi inayoruka yenye kila aina ya vifaa vya teknolojia ya kisasa. Hata hiyo kuna mambo makuu mawili kuhusu Air Force One ambayo watu hawayajui
1." Air Force One" sio ndege": Kwa kifupi ni ishara ya Radio ya mawasiliano ya Jeshi la anga la Marekani wakati Rais wao akiwa angani. Mara tu Rais anapoingia ndani ya ndege, ndege hiyo mara moja huitwa Air Force Once, na wahudumu pamoja na waongoza ndege ili kuepuka mkanganyiko na ndege nyingine yoyote eneo ilipo.
Iwapo Rais atapanda ndege ya kijeshi basi ndege hiyo huitwa “Army One” na hata akipanda chopa yake maalum chopa hiyo huitwa “Marine One”. Watu wengi, hata hivyo watu wengi huiita ndege hiyo kubwa Air Force One.
2. Kwa sasa kuna ndege mbili zinazoruka kwa ishara ya Air Force One--ndege hizo zinafanana sana na ni aina ya Boeing 747-200B zenye namba ya usajiri kwenye mkia 28000 na 29000
Ndege hizo kimuundo zinafanana na ndege za kawaida za boeing 747 na zina uwezo unaofanana. Zina urefu sawa na ghorofa sita. Kila moja ina engine ya jet aina ya CF6-80C2B1 yenye uwezo wa kufua mhimili(thrust) wa pauni 56,700 kila moja. Ndege hizo huweza kusafiri mwendo kasi wa kati ya maili 630 hadi 700 kwa saa na umbali angani wa futi 45,100( Kwa lugha rahisi ndege hiyo kuweza kusafiri kutoka Dar es Salaam mpaka Arusha kwa nusu saa tu). Pia hubeba galoni 53,611 za mafuta na uzito wa pauni 833,000 kwa safari ndefu. Ikiwa imejaa tanki inasemekana ndege hiyo inaweza kusafiri bila kusimama na kumaliza nusu ya ulimwengu mzima.
NDANI YA AIR FORCE ONE
Air force one ina upana wa sakafu wa futi za mraba 4000. Hufanana sana na hoteli ya kifahari kuliko ndege, isipokuwa kitu pekee kinachoifanya ionekane ndege ni mikanda ya kwenye viti. Sehemu ya chini ya ndege mara nyingi hutumiwa kubebea mizigo. Abiria hupanda kwenye sehemu ya katikati, na sehemu ya juu kwa kiasi kikubwa hutumiwa kwa mawasiliano ya kielektroniki.
Rais ana nyumba yake ya kuishi ndani ya ndege hiyo, yenye kitanda, bafu, jimu(gym) na ofisi. Samani nyingi kwenye ndege hiyo zimechongwa kwa mkono na seremara waliobobea.
Ina chumba cha mikutano cha wafanyakazi ofisi ya Rais, kinachotumika pia kama sehemu ya kulia chakula ya Rais. Maofisa wandamizi wana ofisi zao pia ndani ya ndege hiyo, na wafanyakazi wengine wa Rais wana nafasi ya kufanya kazi na kupumzika. Kuna sehemu maalum ya waandishi wa habari wanaosafiri na Rais, kwa ujumla Air Force One inaweza kupakia watu 70 na wahudumu 26
JINSI SAKAFU YAKE ILIVYOPANGWA
Kuna mambo fulani yasiyo ya kweli kuhusu AirForce One. Hata kwa wageni maarufu wanaoitembelea marekani na waandishi wa habari hawaruhusiwi kuingia kwenye baadhi ya maeneo ndani ya ndege hiyo. Jeshi la marekani liko makini sana kuficha baadhi ya taarifa kuhusu jinsi sakafu ya ndege hiyo ilivyopangwa. Maofisa waandamizi wengi wamechapisha maelezo ya ujumla ya kile kilicho ndani ya ndege hiyo, lakini nijuavyo mimi hamna hata mmoja anayejua mpango mzima wa sakafu ya ndege hiyo. Na hata kama wanajua pengine wanaficha ukweli kwa sababu za kiusalama.
Kama Boeing ya kawaida ya 747, Airforce one ina deki tatu. Na kama uonavyo kwenye TV abiria wa Air Force One wanaweza kuingia ndani kwa milango mitatu. Kwa kawaida, kama ilivyokuwa kwa Rais Obama alivyokuja Tanzania bila shaka ulimwona ikipungia mkono watu, hapo ni mlango wa deki ya katikati na ngazi maalumu ilisogezwa karibu na ndege kumuwezesha kushuka. Akina sisi( waandishi wa habari) hutumia mlango wa nyuma kuingia ndani ambapo hupanda ngazi mpaka kufika deki ya katikati. Sehemu wanayoketi waandishi inafanana sana na daraja la kwanza la ndege za kawaida, ikiwa na viti maridhawa na nafasi ya kutosha si kama daraja la akina nyie (uchumi)
VITU VYA KIPEKEE KATIKA AIR FORCE ONE
Kwa kuwa Air force One inambeba Rais , na kwa kuwa baadhi ya safari zake zinaweza kuwa ndefu, ndege hiyo ina vitu kadhaa vya kipekee, vingi vyake havipo kwenye ndege ya kawaida ya Boeing
Wahudumu(Crew) huandaa chakula kwenye jiko maalum lililosheheni mapochopocho ya kila aina. Wanahifadhi chakula kingi kwenye friza iliyopo sehemu ya chini ya ndege. Wapishi wanaweza kuhudumia watu 100 kwa mpigo na sehemu ya kuhifadhi chakula inabeba hadi aina 2000 za vyakula, pengine hata unga wa sembe upo.
Ndege hiyo ina teknolojia nyingi za kisasa kabisa na hospitali. Chumba cha madaktari kina duka la dawa baridi(Pharmacy) kubwa, vifaa vingi vya matibabu ya dharura na hata meza ya kukunja kwa ajili ya upasuaji. Ndege pia ina daktari maalum anayesafiri na Rais popote aendapo. Katika kila safari ndege hiyo huwa imejihami kwa dharura yoyote ile.
Kama isivyokuwa kwa Boeing 747 ya kawaida, ndege hiyo ina ngazi yake maalumu ya kukunjua kwa mlango wa nyuma na mlango wa mbele. Ngazi hizo hutumiwa pia na wahudumu wakiwa ndani ili kupanda mpaka kufikia deki ya katikati. Ndege hii pia ina kifaa maalum cha kupakia mizigo kwa hiyo haitegemei wafanyakazi wa airport kwa sababu za kiusalama.
Kitu pekee cha kushangaza kwenye ndege hii ni mfumo wake wa elektroniki. Ndege hii ina simu 85, Radio koo( kama zile za polisi), nukushi na swichi za kompyuta. Ina TV 19 na vifaa mbalimbali vya ofisi. Simu zinaweza kutumika kupigia watu walio ardhini hata kama iko angani.. Rais na wafanyakazi wake wanaweza kumpigia simu mtu yoyote wakiwa angani.
Mfumu wa elekroniki pia unahusisha maili 238 za waya ( mara mbili ya ndege za kawaida) Uzio mkubwa kwenye waya unatosha kuzilinda na mionzi hatari ya sumaku( electromagnetic) zinazohusiana na mlipuko wa nyuklia.
Ndege hiyo ina uwezo wa kujijaza mafuta ikiwa angani kitu kinachoipa uwezo wa kubaki angani muda wote, kitu ambacho ni muhimu wakati wa dharura.
Mfumo wake wa avionics an usalama ni siri, lakini kama inavyojulikana ndege hizo za airforce one ni ndege za kijeshi, zimetengeneswa kuhimili mashambulizi. Baadhi ya mambo ni kwamba ndege hiyo ina kifaa kujulikanacho kama electronic counter measures(ECM) kinachoweza kudhoofisha mawasiliano ya rada ya adui. Pia ina makombora yanayoilinda dhidi ya adui.
Kila safari ya Air Force One ni safari ya kijeshi, na inachukuliwa hivyo na wafanyakazi wote. Wahudumu wa Andews Air Force Base mjini Maryland huikagua ndege hiyo na njia ya kurukia kabla ya safari yoyote.
Ikiwa tayari kuruka , Chopa ya Marine One humleta rais kutoka White house mpaka kwenye ngome hiyo ya Andrew iliyopo kitongoji cha Maryland Jijini Washington DC.
Askari huwa tayari kuitungua ndege yoyote itakayo zikaribia helikopta za marine One zinazo mbeba Rais.
LikeShow more reactions
Comment

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.