JPM AMTAKA BOSS WA DAWASA AJIPIME AONDOKE


PWANI: Rais John Magufuli amemtaka Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasa) Archado Mtalemwa ajiandae kustaafu kutokana na mapungufu mengi ambayo Rais amesema ameyaona katika mamlaka hiyo.
Rais ameyasema hayo leo(Jumatano) akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani na alitumia fursa hiyo kuzungumzia miradi ya maji na ulipaji wa maji kwa taasisi za serikali.
“Ndugu yangu Mtalemwa, naongea kwa lugha nzuri hapa, nikuombe tu kuwa ustaafu mapema, inawezekana Waziri wa Maji ni rafiki yako, kama ilivyo kwa mawaziri wengine, lakini nadhani huu ni wakati mzuri,” amesema na kuongeza;
“Pamoja na kazi zako nzuri, it’s your time to go.”
 Amezungumzia kero mbalimbali za maji na kusema kuna upotevu mkubwa wa maji. 
Rais amemuagiza Waziri wa Maji, Gerson Lwenge kuhakikisha mradi wa maji wa Ng’apa- Lindi, unakamilika haraka, ikiwezekana waziri ahamie hukohuko.

VIDEO: MSIKILIZE RAIS AKIFUNGUKA

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*