JPM: Mtu Afungwe, Halafu Anunuliwe Chakula? Nimechoka, Nataka Wafungwa Wakalime


Rais John Magufuli amesema ni vizuri magereza yakawa na maeneo mengi ili wafungwa walime na wajue maana ya kufungwa ni nini.
Ameyasema hayo jana (alhamisi) wakati akizungumza wilayani Bagamoyo katika ziara yake ya siku tatu, mkoani Pwani.
 “Nimechoka kuwalisha wafungwa, mtu afungwe halafu anunuliwe chakula. Nimeshatoa maagizo, wafungwa hawa wakalime ili waogope kufungwa,” amesema na kuongeza;
“Wakajifunze kulima, wajue kufungwa ni kufungwa na neno kufungwa ni kufungwa kweli. Tukianza kuwapunguzia maeneo magereza, mnataka wakalime wapi?” amehoji.
Rais amesema, hiyo ndiyo sababu ya kutunza maeneo ya magereza ili yatumike kwa uzalishaji mali.
 Ameongeza kuwa ni vizuri wahalifu wakatumia nguvu kama walizotumia kuiba, ili wakalime.
“Huko magereza wafanye kazi, bila kujali vyeo walivyokuwa navyo, umaarufu wao na wakafanye kazi,” amesema

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI