Korea Kaskazini yarusha kombora la kushambulia meli


Korea Kaskazini ikionyesha makombora ya Styx 2012Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionKorea Kaskazini ikionyesha makombora ya Styx 2012
Korea kaskazini imerusha makombora kadha ya kushambulia meli mashaiki mwa pwani yake, kwa mujibu wa Korea Kusini
Mamlaka zilisema kwa makombora hayo yaliyorushwa Alhamisi asubuhi karibu na mji wa Wonsan yalikuwa ni ya masafa mafupi.
Makombora hayo yaliruka umbali wa kilomita 20o kabla ya kuanguka baharini.
Majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini mwaka huu yamekiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
Wataalamu wana hofu kuwa majaribio hayo na hatua za Korea kutundika silaha za nuklia katika vichwa vya makombora.
Image captionRamani ya Korea Kaskazini
Msemaji wa Jeshi la Korea Kusini amesema kuw majiribio ya hivi punde yalionyesha kuwa Korea Kaskazini ilitaka kuonyesha kuwa ina uwezo wa kulenga meli kubwa baada ya mazoezi ya hivi majuzi kati ya Marekani na vikosi vya Korea Kusini.
Makomboa ya kushambulia meli ni makombora ambayo huelekezwa. Mwaka 2012 Korea Kaskazini ilionyesha makomboa kadha kama hayo yanayojulikana kama Styx.
Lakini hapo awali Korea ilijaribu bila mafanikio kufanyia majaribio makombora ya kushambulia meli.
Image captionMarekani inaweka mitambo ya kujikinga nchini Korea Kusini

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA