Mabaki ya ndege ya Myanmar na maiti za abiria zapatikana baharini


Picha ya maktaba ya ndege ya jeshi la angani la Myanmar muundo wa Y-8Haki miliki ya pichaAFP
Image captionPicha ya maktaba ya ndege ya jeshi la angani la Myanmar muundo wa Y-8
Jeshi la Burma limesema kuwa mabaki ya ndege yake iliyotoweka Jumatano katika anga ya bahari ya Andaman ikiwa abiria 122 wengi wao wanajeshi na familia zao, yamepatikana.
Mabaki ya ndege na maiti zimepatikana katika bahari ya Andaman, kwa mujibu wa taarafa iliyotolewa na idara ya jeshi.
Ndege hiyo aina ya Y8, iliyotengezwa nchini China, ilikuwa na wahudumu 14 pamoja na wanajeshi 106 na familia wakiwemo watoto.
Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka Myeik ikielekea Yangon.
Ndege hiyo ilikuwa imefanya safari ya nusu saa, wakati ilipoteza mawasiliano siku ya Jumatano.
A map showing Myeik, Dawei, and Yangon in Myanmar
Image captionMyeik, Dawei, na Yangon nchini Myanmar
Ndege hiyo ilinunuliwa kutoka China mwezi Machi mwaka uliopita na tayari ilikuwa imeruka kwa saa 809.
Mynmar imekumbwa na ajali kadha za ndege miaka ya hivi karibuni. Lakini ajali hii ya sasa ndio mbaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo.
Mwezi Februari mwaka 2016 watu watano waliokuwa wakisafiri wakitumia ndege ya jeshi, walifariki wakati ndege yao kuanguka kwenye mji mkuu wa Nay Pyi Taw.
Miezi mitatu baadaye maafisa watatu, waliuwawa wakati helikopta ya jeshi ilipoanguka kati kati mwa Mynmar.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NAMAINGO YAZINDUA HEKA 7000 ZA MASHAMBA MJI KIJIJI CHA MSOLWA, MKURANGA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

HABARI MPASUKOOO:GARI LAGONGA WATOTO KUIKWEPA BODABODA GONGO LA MBOTO

HARAMBEE YA UJENZI HOSPITALI YA MUHEZA YAVUKA MALENGO, ZAPATIKA BIL. 1.6

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

WAZIRI SHONZA AMJIBU DIAMOND

HABARI MPASUKOOO!!! MCHAWI ADONDOKA AKIWA UCHI KIVULE,DAR

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI