Mama Amkata Uume MtotoUKATILI wa kutisha! Hakuna lugha ny­ingine unayoweza kuzungumza zaidi ya kusema hivyo, baada ya mama mmoja, mkazi wa Sinza C jijini Dar es Salaam, ku­kata uume wa mtoto wa jirani yake, kwa madai kuwa alimbaka binti yake wakati wakicheza sebuleni, Risa­si Jumamosi limetonywa.

Inadaiwa kuwa mtoto aliyepatwa na maswaibu hayo, Richard mwenye umri wa miaka minne, alikuwa sebuleni akicheza na binti aliyefahamika kwa jina moja la Abby (3) kabla ya mama mwenye nyumba kurejea na kushangaa kumuona bintiye akiwa na tone la damu kwenye nguo zake.

Akizungumza na paparazi wetu, baba wa Richard, Paul Konyaki alisema alipewa taarifa na majirani wa mtaa wa pili siku chache zilizopita kuwa mtoto wake amekatwa sehemu za siri na mama huyo.


“Huyo mama alipotoka kazini alimkuta mtoto wake ana tone la damu kwenye nguo, ndipo akaanza kumbana mtoto wangu kamfanya nini mwenzake na kuanza kumuadabisha kwa kumkata na kisu sehemu ya mbele ya uume wake akidai kambaka mwanaye.

“Ni kitendo ambacho kilinistaajabisha maana wale wote ni watoto na aliwakuta wamekaa tu, si kwamba aliwashuhudia wakifanya uchafu na nyumba hiyo ilikuwa na dada wa kazi, sasa kama kuna utundu ulifanyika hadi yule mtoto kuumia akatoka damu, si angemsikia akilia, lakini haikuwa hivyo,” alisema.

Akiwa na jazba, baba huyo alisema, jambo hilo lilimkera kwani ni ukatili uliokithiri, hivyo akaanza ku­haha kutafuta anapoishi na akafanikiwa kupajua kwa msaada wa majirani ambao wanamfahamu.

“Nilipofika pale badala awe mpole kwa ukatili ali­oufanya, akaanza kunitambia kuwa yeye anafanya kazi serikalini, siwezi kumfanya chochote na kunilau­mu kuwa sijamlea vyema mwanangu, nikaona huyu atanisababishia matatizo mengine, nikaachana naye.

“Nikaenda polisi kuchukua PF3 kisha nikaenda Hospitali ya Palestina ambapo madaktari walishauri wamfanyie tohara kabisa kutokana na hali aliyokuwa nayo ili kumnusuru tatizo lisiwe kubwa zaidi, taratibu za kisheria zinaendelea hadi tufikishane mahakama­ni,” aliongeza.

Kwa upande wake, mtoto huyo aliyefanyiwa un­yama huo alisema; “Mama yake alivyorudi kazini alitukuta tunaangalia katuni akaanza kunifinya na kunikata huku na kisu, yule baba yake Abby akasema msamehe yeye hataki, akaniambia wee usije tena kucheza na mtoto wangu.”

Risasi Jumamosi lilimtafuta mwanamke huyo kwa njia ya simu, lakini namba yake haikuweza kupatika­na hewani, lakini alipopatikana mumewe, alisikiliza tuhuma hizo mwanzo mwisho na alipotakiwa kuse­ma chochote, alikata simu.

Shauri hilo limeripotiwa katika Kituo cha Polisi Mabatini (Kijitonyama) na kuandikiwa jalada lenye namba KJN/RB/6258/17 SHAMBULIO 08/06/17.j
STORI: MAYASA MARIWATA, RISASI JUMAMOSI
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA