4x4

MAYANGA: TUTAZINDUKA NA TUTASIMAMA IMARA TENA


Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Mayanga amesema watazinduka na kufanya vizuri katika mechi zijazo za Kundi L kufuzu Fainali za kombe ka mtaifa ya Afrika mwaka 2019.
Taifa Stars ilianza vibaya mbio za Cameroon 2019 usiku wa jana, baada ya kulazimishwa sare ya nyumbani 1-1 na Mamba wa Lesotho katika mchezo wa kwanza wa Kundi L Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. 
Na baada ya mechi katika mkutano na Waandishi wa Habari, Mayanga akalaanu kitendo cha safu yake ya ulinzi kuruhusu bao la kusawazisha la Lesotho lililofungwa Thapelo Tale dakika  ya 34, kufuatia Nahodha wa Tanzania, Mbwana Samatta kufunga la kuongoza dakika ya 27.
Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga amesema timu itazinduka na kufanya vizuri tena

“Tumefanya makosa kuruhusu goli rahisi la Lesotho, lakini sare ya leo haitukatishi tamaa na tutaendelea na mazoezi kama kawaida kwa ajili ya mechi zilizosalia. Naamini makosa ya  leo tutayafanyia kazi na tutazinduka, tutafanya vizuri,”amesema Mayanga. 
Kocha huyo aliyerithi mikoba ya mzalendo mwenzake, Charles Boniface Mkwasa ameongeza kwamba Lesotho jana walikuwa wanatumia mbinu ambazo ni changamoto kwake na atazifanyia kazi.

Post a Comment