MJADALA WA BHANGI WATAWALA BUNGENI LEO

Bhangi ikiteketezwa 

Mjadala wa Mmea wa Bhang umetawala leo bungeni kwa kusababisha mvutano baina ya wabunge waliokuwa wakitetea matumizi ya mmea huo na upande wa serikali ambao unapiga marufuku.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee,  Dk. Khamisi Kigangwala, alijibu kuwa bhangi  na sawa na dawa za kulevya ambazo kisheria yamepigwa marukuku nchini.

Alisema kuwa baadhi ya maeneo wasijidanganye kwamba mtu akivuta bhang hulima shamba kama trekta. alisema kuwa mmea huo una madhara kwa afya ya binadamu na endapo mtu mmoja akionja mara moja basi hukaa mwili kwa muda wa siku saba na kutoweka na enedapo atavuta mara nyingi basi itakuwa ni klonic na kumsababishia madhara ya kiafa na kiakili.

Spika wa Bunge, Job Ndugai  aliingilia kati kwa kumpa nafasi mmoja wa wabunge wanaotoka  eneo linalolima bhangi kwa wingi, ambapo nafasi hiyo aliipata Mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiku, ambaye alionekana kuitetea bhangi kuwa endapo ina athari hawaoni askari wanaoshiriki kuteketeza wanaathiriwa na moshi ndo sababu wanaboronga kazi zao.

Dk. Kigangwala alijibu kuwa kwa askari haina madhara kwani wanapoiteketeza huvaa usoni vifaa vya kuzuia moshi, jambo ambalo lilizua mguno kutoka kwa wabunge ambao walionesha dhahiri kutokubaliana na jibu hilo kwani mara nyingi askari wanapoteketeza bhangi hawvai vifaa hivyo.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MAMEYA WA TEMEKE, UBUNGO WATWANGANA UCHAGUZI WA NAIBU MEYA DAR

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

RAIS MSTAAFU KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA MWANAHABARI ATHUMAN HAMISI DAR