Msafara wa Sumaye Wazuiliwa, Meya wa Ubungo Achukuliwa na Polisi


DAR ES SALAA: Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amechukuliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano hata hivyo sababu za kuchukuliwa kwake bado hazijawekwa wazi.
Tukio limetokea leo Jumatatu saa sita mchana katika makao makuu ya wilaya hiyo yaliyopo Kibamba.
Askari wapatao wanne wakiwa katika gari aina ya Land Cruise walifika katika eneo hilo kisha kuzuia msafara wa viongozi wa Chadema waliokuwa tayari kuanza ziara ya kutembelea manispaa hiyo.
Miongoni mwa viongozi hao wa Chadema ni waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na viongozi wengie wa Ubungo na Kanda ya Pwani.
Baada ya kuzuia msafara huo, mmoja wa askari alishuka na kumfuata Jacob na kumweleza anamuhitaji kuambatana naye hadi Kituo cha Polisi cha Mbezi.
“Tunakuomba uongozane na sisi hadi kituoni tuna maongezi na wewe yasiyozidi dakika 10 tukiridhika tunakuachia uendelee na shughuli zako,”
Baada ya kumweleza hayo, ofisa huyo alikwenda moja kwa moja katika gari la Sumaye na kumweleza kuwa wanamuhitaji meya kwa dakika 10 kisha watamuachia.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*