MSIKILIZE JPM AKIPINGA WANAFUNZI WENYE MIMBA KUENDELEA NA MASOMO


PWANI: Rais John Magufuli amesema ndani ya wa utawala wake kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hakuna mwanafunzi atakayepata mimba na kuruhusiwa kurudi shule.
 Ameyasema hayo leo (Alhamisi) wakati wa ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani ambako amezindua viwanda saba.
“Azae halafu aende kuwahubiria wenzake, unajua ilikuwa hivi, halafu nilifanya hivi,”amesema.
Amesema waliozaa shuleni wanaweza kwenda kupata elimu nyingine kama vyuo vya ufundi stadi (Veta) na kilimo badala ya kurudi shule na kuanza kuwafundisha wenzao yale waliyoyafanya.
“Mnataka niwaambie warudi shule halafu, ni bora wakalime ili ile nguvu waliyoitumia kujifungua waitumie kulima,” amesema.
Amesema; “Ni rahisi zaidi kuzalia chuo kikuu, ule mwaka wa kwanza, wa pili lakini sekondari, darasa la kwanza  kupeleka walio na watoto, tunapoteza maadili yetu, watazaa mno.”
 “Mtajikuta darasa la kwanza wote wanawahi nyumbani kwenda kunyonyesha. Hii tutalipeleka Taifa pabaya,” amesema.

MSIKIE JPM AKITOA KAULI HIYO


Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.