Msuva Akataa Mshahara wa Mil 9 Kwa Mwezi


Mchezaji wa Yanga, Simon Msuva.
OFA ya Simon Msuva kwenda Morocco imekamilika na klabu ya Difaa El Jajida kutoka nchini humo iko tayari kumwaga dola 4,000 (takriban Sh milioni 9) kumlipa mshahara kila mwezi. Lakini taarifa zinaeleza Msuva amekataa kupokea mshahara
huo wa Sh milioni 9 akisema ni kidogo na alivyokuwa akitarajia. Difaa El Jajida ni timu ya Ligi Kuu nchini Morocco na msimu ujao itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kushika nafasi ya pili, mabingwa wakiwa Waydad Casablanca. Habari za uhakika kutoka Morocco zinaeleza, Msuva amesema mshahara huo ni mdogo.
“Tumeelezwa hivyo kwamba amekataa dola 4,000 ni kidogo. Pia timu yake haitaki kupokea dola 80,000 (takriban Sh milioni 177) kumuuza,” alisema Mohamed El Hamsi, mmoja wa mawakala nchini Morocco. “Mimi ushauri wangu waambie kuwa Tanzania haina soko huku Afrika ya Kaskazini, vizuri aje acheze na baada ya hapo
anaweza kutanua soko. “Naona si sahihi kukataa ofa hiyo, Yanga wamesema hadi dola 130,000 (zaidi ya Sh milioni 287). Nafikiri si sawa, ikiendelea hivyo baada ya siku chache tutaangalia Msenegal au Mmali mmoja ambao pia wanasubiri.” Juhudi za kumpata Msuva hazikufanikiwa kwa kuwa
yuko nchini Afrika Kusini akiwa na kikosi cha Taifa Stars kinachoshiriki michuano ya Cosafa. Hivi karibuni, Msuva alizungumza na gazeti hili na kueleza alikuwa na ofa tatu kutoka Afrika Kusini, Misri na Morocco na alikuwa tayari kwenda kokote kulingana na ofa
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

WAKIANGALIA MATOKEO YA DARASA LA SABA, MBOZI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

JK AWATUNUKU WANAFUNZI 1400 DUCE DAR ES SALAAM