Mtu Mmoja Akamatwa Akiingiza Nyama Zikiwa na Smart Phones 5 Kwa Wafungwa Gereza la Keko


DAR: Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Nombo mkazi wa Dar, amekamatwa leo Juni 19, 2017 akijaribu kuingiza simu 5 katika Gereza la Mahabusu la Keko.
Kijana huyo alikuwa amezifunga simu hizo kwenye mapande ya nyama yaliyorostiwa kama inavyoonesha kwenye picha. Simu hizo zilikuwa ziingizwe gerezani humo ili wapewe wafungwa kwa ajili ya mawasiliano jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Global Publishers imefanya jitihada za kumtafuta Kamanda wa Magereza wa Mkoa wa Dar, DCP Mboje ambaye amethibitisha kukamatwa kwa kijana na kusema kuwa amepelekwa polisi ili achukuliwe hatua za kisheria.
Taarifa zaidi za tukio hilo la aina yake usikose nakala yako ya Uwazi kesho Jumanne.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*