MUZAMIL MCHEZAJI BORA STARS IKITOA SARE 0-0 NA ANGOLA COSAFA


Na Mwandishi Wetu, RUSTENBURG
KIUNGO wa Simba, Muzamil Yassin Said amekuwa mchezaji Bora wa mechi ya pili ya Kundi A, Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika, COSAFA Castle 2017, Tanzania ikitoa sare ya 0-0 na Angola Uwanja wa Royal Bafokeng mjini Rusternburg, Afrika Kusini usiku wa leo.
Zilikuwa dakika 90 ngumu, ikishuhudiwa timu zote zikishambuliana kwa zamu na wachezaji wa timu zote wakionyesha umakini wa hali ya juu.
Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga alibadilisha karibu safu yote ya ushambuliaji kipindi cha pili akiwatoa Simon Msuva, Shiza Kichuya na Elias Maguri, ambao nafasi zao zilichukuliwa na Mbaraka Yussuf, Thomas Ulimwengu na Stahmili Mbonde – lakini matokeo yakagoma kubadilika.
Muzamil Yassin amekuwa mchezaji bora wa mechi, Tanzania ikilazimishwa sare ya 0-0 na Angola leo

 Kwa matokeo hayo, Tanzania inaendelea kuongoza Kundi A ikifikisha pointi nne baada ya ushindi wa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Malawi, mabao yote akifunga Shiza Kichuya Jumapili, wakati Angola iliyoifunga 1-0 Mauritius katika mchezo wa kwanza ni ya pili.
Malawi baada ya sare ya 1-1 na Mauritius leo, inakwenda mkiani mwa kundi hilo. Mechi za mwisho za kundi hilo zitachezwa kesho kubwa, Tanzania ikimaliza na Mauritius na Angola na Malawi katika mchezo unaotarajiwa kuwa mkali zaidi.  
Kundi B lina timu za Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe na mshindi wa kwanza wa kila kundi atakwenda hatua ya Robo Fainali kuungana na Botswana, Zambia na Afrika Kusini, Namibia, Lesotho na Swaziland, zinazoanzia hatua hiyo.
Kikosi cha Tanzania leo kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Gardiel Michael, Salim Mbonde, Abdi Banda, Himid Mao, Erasto Nyoni, Simon Msuva/Mbaraka Yussuf dk68, Muzamil Yassin, Elias Maguri/Stahmili Mbonde dk89 na Shiza Kichuya/Thomas Ulimwengu dk74.
Angola; Gerson Barros, Lunguinha, Wilson, Dani Masunguna, Natael/To Carneiro dk23, Paty, Herenilson, Dudu Leite, Nelson, Caporal na Amaro/Carlinhos dk76.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI