4x4

Mzee Mwinyi Aongoza Swala ya Eid El Fitr Dar


Mzee Ali Hassan Mwinyi (KUSHOTO) akijumuika na waumini wengine wa Dini ya Kiislam katika swala ya Eid El Fitr iliyoswaliwa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar esa Salaam.

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, mapema leo Jumatatu amewaongoza waumini wa Kiislamu katika kusherehekea Sikukuu ya Eid El Fitr, katika swala ya Eid El Fitr  iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salum akitoa nasaha zake kwa waumini wa dini ya Kiislamu.

Akizungumza na waumini mara baada ya swala hiyo, mzee Mwinyi aliwataka Waislamu  wote nchini kusherehekea sikukuu hiyo kwa kufanya matendo mema ya kumpendeza Mwenyezi Mungu.

Taswira ya baadhi ya waumini waliojitokeza katika Viwanja vya Mnazi Mmoja inavyoonekana.

“Waumini wa Dini ya Kiislam muendeleze ushirikiano,umoja na mshikamano na madhehebu mengine ya dini nchini, pia mwendeleze kudumisha matendo mema kama mlivyofanya kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani,”alisema.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Salim Ahmed Salim akimsalimia mzee Mwinyi.

Waumini wakiomba dua.

Kamishna Mstaafu wa Kanda Maalum Dar es Salaam, CP Suleiman Kova naye akijumuika na waumini wa dini hiyo katika dua.


Sehemu ya waumini akinamama waliojitokeza katika swala hiyo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja
Mwinyi akitoa hotuba yakle kwenye swala hiyo.
Post a Comment