NAIBU SPIKA DK. TULIA ATEMBELEA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE


 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimpokea  Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Tulia Ackson alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto  wanawaosubiri kufanyiwa upasuaji.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya
 Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi  (kulia) akizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Tulia Ackson jinsi wanavyotoa  huduma za matibabu ya magonjwa ya Moyo wakati alipotembelea Taasisi hiyo jana Juni 10, 2017 kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wanawaosubiri kufanyiwa upasuaji.
 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akimjulia hali  mtoto Doreen Sostenes (3) ambaye Taasisi ya  Tulia Trust Fund imemlipia gharama za matibabu ya upasuaji wa Moyo ambao utafanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Kulia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto Naiz Majani.
 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiwa amembeba   mtoto Doreen Sosthenes (3) ambaye Taasisi ya Tulia Trust Fund imemlipia gharama za matibabu ya upasuaji wa Moyo ambao utafanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akimtazama mtoto Johnson Raphael (6) akichora picha ya mtu wakati alipotembelea  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jana Juni 10, 2017 wakati alipofika katika Taasisi hiyo kwa lengo la kuwajulia hali  watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji. Kulia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto Naiz Majani.
 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson (kulia) akiwa amembeba mtoto Zuwena Said (4) aliyelazwa katika   Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kusubiri upasuaji wa Moyo. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto Naiz Majani.
 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akimjulia hali mtoto Abdukarim Mahilo (2)  aliyelazwa katika   Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kusubiri kufanyiwa upasuaji wa Moyo huku Mama wa mtoto Fatuma Bakari akiangalia.
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akiongea na Maria Gervas  ambaye ni mama wa Doreen Sosthenes (3) anayelipiwa gharama za upasuaji wa  Moyo na Taasisi ya Tulia Trust Fund. Dkt. Tulia alitembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)  leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji.

 Daktari Bingwa Magonjwa ya Moyo kwa Watoto Taasisi ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Mkuu wa Idara Dkt Sulende Kubhoja (kushoto) akizungumzia magonjwa mbalimbali ya moyo yanavyowasumbua watoto wakati  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson      alilipotembelea  Taasisi hiyo  jana kwa kuwajulia hali watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji.
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson (kulia) akimjuliaa mtoto Venance  Christopher (14) aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kusubiri upasuaji wa  Moyo Dkt. Tulia alitembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto  hao
 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson (kulia) akizungumza jambo na Rashid Kombo aliyelazwa chumba cha uangalizi maalum (ICU) baada ya kufanyiwa upasuaji wa Moyo. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi hiyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani akifuatiwa na  Daktari Bingwa wa Moyo kwa watoto na Mkuu wa Idara ya Magonjwa hayo ya Moy Dkt. Sulende Kubhoja. 
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akimsikiliza Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kwa Watoto na Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Moyo kwa Watoto Godwin Sharau mara alipotembelea watoto na kufika katika chumba cha upasuaji wa Moyo kilichopo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwetwe (JKCI). (PICHA ZOTE NA ANNA NKINDA WA JKCI)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI