NDANI YA GBADOLITE, JIJI BINAFSI LA MOBUTU LILILOJIFICHA KWENYE MSITU MNENE KASKAZINI MWA KONGO


• Harusi ya Binti wa Mobutu ilipambwa na wageni 7500
• Keki iliagizwa Ufaransa Kwa ndege Maalum
• Gauni iligarimu Dola za Kimarekani 75,000
• Mikufu ya almas, iligarimu dola million 3
Kwa miaka tisa Olela Shungu alihudumu kama mfasiri binafsi wa mdhalimu Mobutu na mara nyingi alitembelea Gbadolite, kasri la Rais lililojificha kwenye msitu mnene kaskazini mwa Leopoldvile au Kongo DRC kama inavyojulikana kwa sasa, Kasri hilo lililosheheni kila aina ya anasa lilipewa jina la ‘ Versailles in the Jungle’ likifananishwa na Mji maarufu uliopo kaskazini wa Ufaransa na Kusini Magharibi mwa Paris, unaojulikana kwa majumba ya kifahari ya mfalme, yaliyojengwa na Mfalme Louis XIV mwishoni mwa mwaka 1600 na ndipo haswa mkataba wa makubaliano kumaliza vita ya dunia ya kwanza mwaka 1919 ulisainiwa.
Miaka ishirini baada ya kifo cha ‘Mfalme wa Ajabu’ Mobutu Seseseko, fahari yote katika Kasri la Gbadolite ikiwemo samani zilizochongwa kwa ustadi na seremara maarufu duniani, na kila aina ya nakishi pesa za wizi zinavyoweza kununua, ililala.
Endelea…..
Na Kizito Makoye, kwa msaada wa vitabu na majarida mbalimbali duniani
“Ndiyo, Ningali Hai,” Alisema Oleal Shungu huku akitabasamu, wakati akielezea miaka tisa aliyofanya kazi kama mfasiri binafsi wa Mdharimu katili kabisa duniani Mobutu Sese Seko
Shungu, aliyeonwa na jicho la husuda la Mobutu wakati wa kazi yake kama miongoni mwa wafasiri rasmi wakati wa Pambano la Mohammad Ali na mpinzani wake George Foreman, lililojulikana kama Rumble in the Junge mwaka 1974, baadae alimsindikiza Mobutu kila aendapo wakati wa ziara za ndani na za nje ya nchi.
Njiani, alijaza zaidi ya pasi za kusafiria 20 na kukutana na Marais wa nchi wasiohesabika pamoja na watu mashuhuri kadhaa.
Safari za Shungu maranjingi zilimfanya afike Gbadolite, kasri la kifahari la Mobutu lililopo ndani ya msitu mnene kaskazini mwa DRC.
Kama nilivyoeleza awali, Kasri hilo lilijulikana kama Versailles in the Jungle likifananishwa na mji maarufu nchini Ufaransa. Kiukweli Gbadolite lilikuwa ni zoezi la ziada, huku kukiwa na makasri matatu tofauti ya mfalme Mobutu yaliyosheheni samani na urembo wa kila aina ikiwemo, nyumba za kulala wageni( siyo gesti kama za dar ambazo mtu analala kwa masaa mawili anaondoka), sehemu ya michezo, ukumbi wa disco, pia kwa kuwa eneo hilo lilikuwa karibu na Mto Congo, unaomiminika kwa madoido kiasi cha kuwafanya tumbili kwenye misitu kukata viuno kila wasikiapo mziki wa Ndombolo kutoka moja ya ukumbi wa disco, Gbadolite ilikuwa na mtambo wake binafsi wa kuzalisha umeme wa maji( hydro-power). Pia Kasri hilo lilikuwa na uwanja binafsi wa ndege wa kimataifa wenye barabara ya kurukia ndege yenye uwezo wa kuhudumia ndege aina ya Concorde, ambazo Mobutu mara kwa mara alizikodi kwa ajili ya kufanya shopping hasa ya shampeni (Champagne) nyekundu na Maua kutoka Uholanzi.
Kwa vijana ambao hamjui Ndege za concorde, zilitengenezwa Mjini Tolouise Ufaransa na ziliamrishwa kutoruka baada ya matatizo ya kiufundi kwenye mfumo wake wa Avionics(virusha ndege) zilifanana na ndege aitwae Vulture, yule anayenyemelea mizoga!
“ Nilienda huko mwanzo kabisa, wakati Gbadolite haikuwa kitu zaidi ya msitu mnene,” Shungu anasema. “ Baada ya hapo ilibadilika kuwa mji mzuri sana. Na kulikuwa na tafrija nyingi sana, nyingi mno. Wakati mwingine ikiwa kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa, au siku ya Kuzaliwa ya mkewe Antoneite. Na cha kushangaza wakati mwingine serikali yote iliruka kwa ndege kuja Gbadolite na kurudi Kinshasa”
Gbadolite ilijivunia minara ya pagoda na vijiji vya Potemkin kama vilivyopo china, vilivyosheheni ng’ombe na kondoo walioletwa kutoka nje. Misururu ya magari ya kifahari aina ya Mercedes Benz yalisafirisha wageni kutoka uwanja wa ndege na kumbi mbalimbali za starehe huko Gbadolite, huku wageni wakivinjari manthari tulivi iliyopambwa na bustani zenye fonteni za maji yanayoruka juu kutengeneza umbo la maua huku ndege tausi wale kama wa Ikulu ya JPM wakichanua na kudhihirisha utukufu wa mwenyezi Mungu kandokando ya vitanda maalum vya kutengeneza miguu na kucha( Manicure) kwa anayependa.
Moja ya shughuli ya anasa ilifanyika mwaka 1992, wakati huo mimi nilikuwa mwanafunzi wa sekondari Tabora, wakati mtoto wa kike wa Mobutu aliyejulikana kama Yakpwa alipoolewa, au ‘Yaki’ kwa kweli kwa sura na umbile alifanana sana na rafiki yangu mmoja humu facebook anaitwa Maria Mbarikiwa. Alivaa gauni linalokadiriwa kuwa na thamani ya $ 70,000( Pesa za kitanzania zaidi ya Milioni 120) huku likinakishiwa na seti ya mikufu ya almasi yenye thamani ya dola $3 milion ikiwa ni zawadi kutoka kwa baba yake.
Zaidi ya wageni 2500 waliokula mlo wa wadudu wa baharini wanaoitwa (lobster) na mayai ya samaki yaliyopikwa kwa ustadi na kuchanganywa na chumvi. Kwa Mliofika Zanzibar mnaweza kukumbuka wadudu hao huuzwa pale forodhani kwenye mbatata urojo. Wageni pia walishushia mlo huo kwa shampeni nyekundu, na zaidi ya chupa elf moja za wine(waini) bora zaidi iliyopikwa Ufaransa, kabla ya kuanza kumumunya keki maalum ya harusi iliyonunuliwa Ufaransa kwenye ndege maalumu ya kukodi.
Mobutu aliijenga sana Gbadolite kwa kuwa ndipo alipokulia, Shungu anasema: “ Alikuwa anawahimiza wanasiasa wote wanaofanya kazi nae,” Lazima muanzie mlikotoka. Ndiyo maana nafanya haya hapa Gbadolite. Fanyeni hivyo nyumbani kwenu pia.”
Alisema kwamba huku wanakijiji wa Gbadolite walifurahishwa na Kujengeka kwa mji wao, matanuzi ya Mobutu na wafuasi wake hayakuwanufaisha chochote zaidi ya kuambulia mlio wa bilauri zinazogongana harufu ya mapochopocho kutoka viunga vya ikulu.
“ Watu wengi walikasirishwa sana, kwanini anatengeneza ufahari wote huo msituni badala ya kujenga miji mingine iliyopo Kongo, Kwa nini? Tuna miji kama Mbandaka, ambao ni mji mkuu kwenye jimbo la Ikweta, Kwa nini asiujenge huo badala ya kuharibu fedha kujenga msituni? Hapana, watu walikasirishwa mno”
Kuvinjari kwa Shungu hakukukosa hatari. “ Nakumbuka siku moja , tukikuwa tunakutana na Rais wa Zambia Kenneth Kaunda. Kwenye mahojiano hayo tulikuwa wane tu; marais wawili, mimi na mfasiri wa Rais Kaunda, ambaye alikuwa ni mpwa wa Rais Kaunda. Alimuuliza Mobutu “ Huyu ni mtoto wa dada yangu, Namwamini. Naweza kuzungumza kwa uhuru, je unamwamini mfasiri wako?
“ Kwa kweli lilikuwa swali gumu sana,” Shungu anasema. “ Mobutu alikuwa na kuongea na mimi kwa Lingala na aliniambia , ‘ Olea, kama unafanya kazi na mimi na unatoa siri zangi nje, itakuwa kitu kibaya sana’ Shungu anasema
“ Alimaanisha ukizungumza nitakuua. Aliongea kwa tabasamu lakini kwa kweli niliogopa sana. Baada ya hapo Mobutu akamwambia Kaunda Hamna tatizo ongea kwa uhuru.
“ Kila mtu aliniamba kuwa makini. Mobutu atakumaliza. Wakati mwingine anaua watu. Kuwa makini. Kwa nini usiache kazi hiyo?’ Niliogopa sana—hata hivyo ningefanyaje? Nilihitajika niwe pale. Lakini ilikuwa hatari mno kwa yale niliyoyasikia. Wakati mwingine nilirudi nyumbani na kushindwa kabisa kula. Mke wangu aliniambia “ Bebi(baby) njoo ule chakula dia(dear). Kula. Na nikasema, Hapana nitakula kesho,” alisisitiza Shungu kwa masikitiko.
Kama ilivyokuwa kwa Mobutu, Gbadolite haikushinda majaribu ya muda. Wahuni waliivamia Rais Mobutu alivyopinduliwa. Kilichofuatia ni wimbi kuu la uharibifu mali na wizi kwenye majengo hayo ya kifahari uliofanywa na waasi wakiongozwa na Laurent Kabila baba yake Rais Kabila wa sasa ambaye alishawahi kuishi Dar es salaam na anajua Kiswahili pengine kuliko sisi waswahili wenyewe. Msitu huo wa Gbadolite ukamaliza kazi yake.
“ Gbadolite kwa sasa ni msitu mnene,” Shungu anasema. Alivyoulizwa anafikiri nini kuhusu anasa za bosi wake wa zamani, Shungu anainama na kuchukua muda kidogo kujibu…” Nadhani,” alisema, kabla hajaripuka kwa kicheko “ Sitaki kusema ilikuwa ni upuuzi mtupu, ilikuwa ni ushenzi mtupu
Shukrani za kipekee kwa Rafiki yangu na Mwandishi Thomas Yocum na mtunzi wa kitabu cha Loba Lingala
Usikose simulizi itakayofuatia Jinsi Kifo cha Rais Habyarimana wa Rwanda aliyekuwa amesafiri kwa ndege kutoka Dar es salaam alipokuwa na mazungumzo na Mzee Ruksa….kilivyomuuma Mobutu… Tafadhari share Makala hii!
LikeShow more reactions
Comment

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA