4x4

Ngoma kurudi Ijumaa kumaliza ubishi

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Klabu ya Yanga, Donald Ngoma anatarajia kurejea nchini Ijumaa tayari kwaajili ya kusaini mkataba mpya na klabu hiyo. Mbali na Ngoma pia timu hiyo, inatarajia kumpokea Kocha wao Mkuu Mzambia, George Lwandamina siku hiyo akitokea nchini kwao alikokwenda kwa mapumziko. Kumekuwa na taarifa tofauti zikimuhisisha Ngoma kutakiwa na timu ya Simba kitu ambacho kimeongeza presha kwa Yanga ikizingatiwa amemaliza mkataba wake. Akizungumza na gazeti hili, Mjumbe
wa Kamati ya Usajili wa klabu hiyo, Hussein Nyika alisema tayari wameshamalizana na mshambuliaji wao Ngoma ambaye Ijumaa anatarajia kuwasili kwaajili ya kusaini mkataba. “Tumeshamalizana na Ngoma, Ijumaa anatarajia kuwasili nchini kwaajili ya kusaini mkataba mpya, kitu kikubwa ambacho kilikuwa kinasumbua mchezaji alihitaji kuboreshewa maslahi yake kwenye mkataba mpya na tunamshukuru Mungu tumefanikisha,” alisema. “Tunatambua uwezo wake na kuthamini mchango wake, tumeamua kumtimizia mahitaji yake lengo likiwa ni kuhakikisha kikosi kinabaki katika ubora wake kama misimu mitatu
iliyopita,” alisema. Alisema timu hiyo imekuwa ikisikia tetesi mbalimbali kutoka kwa watani wao wa jadi, Simba wakiwania saini ya mchezaji huyo hivyo wamepambana kuhakikisha awampotezi. Akizungumzia suala la kocha, atarejea Ijumaa na atapata mapumziko ya muda na Julai 3, mwaka huu ataanza rasmi kukinoa kikosi kwaajili ya msimu ujao wa ligi. “Ujio wa kocha mapema utakuwa na maana kubwa kwani atasaidia kujaza nafasi za usajili ambazo zitakuwa bado hazijakamilika na kuweza kutoa mawazo mapana ambayo yatasaidia kuboresha kikosi cha ushindani,” alisema.

Post a Comment