OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YAWAPIGA MSASA MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI KUHUSU SHERIA YA TAKWIMU YA MWAKA 2015
Mwanasheria wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu, Oscar Mangula akiwasilisha mada inayohusu Sheria mpya ya Takwimu ya
mwaka 2015 wakati wa mafunzo kwa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini yaliyofanyika
leo mkoani Morogoro kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa
kuifahamu Sheria
mpya ya Takwimu ya mwaka 2015.
Meneja wa Idara ya Mbinu za
kitakwimu, Viwango na Uratibu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Emilian
Karugendo akitoa ufafanuzi wa namna Ofisi ya Taifa ya Takwimu inavyokusanya
takwimu rasmi nchini kwa kuzingatia kanuni za kitaifa na kimataifa wakati wa
mafunzo kwa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini yaliyofanyika leo mkoani
Morogoro kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuifahamu
Sheria mpya
ya Takwimu ya mwaka 2015.
: Baadhi ya Maafisa Habari na Mawasiliano
Serikalini wakifuatilia uwasilishwaji wa mada wakati wa mafunzo kwa Maafisa hao
yaliyofanyika leo mkoani Morogoro kwa ajili ya kuwajengea
uwezo wa kuifahamu Sheria
mpya ya Takwimu ya mwaka 2015.
: Baadhi ya Maafisa Habari na Mawasiliano
Serikalini wakifuatilia uwasilishwaji wa mada wakati wa mafunzo kwa Maafisa hao
yaliyofanyika leo mkoani Morogoro kwa ajili ya kuwajengea
uwezo wa kuifahamu Sheria
mpya ya Takwimu ya mwaka 2015.
Na:
Emmanuel Ghula
Morogoro
1
Juni, 2017.
OFISI
ya Taifa ya Takwimu (NBS) imetoa mafunzo kwa Maafisa Habari na Mawasiliano
Serikalini leo mkoani Morogoro kuhusu Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 ili
kuwajengea uwezo wa kufahamu namna sheria hiyo inavyofanya kazi.
Akifafanua
sheria hiyo, Mwanasheria wa NBS, Oscar Mangula amesema sheria ya Takwimu No. 9
ya mwaka 2015 imeipa Ofisi ya Taifa ya Takwimu jukumu la kuratibu na kusimamia
ukusanyaji wa takwimu rasmi nchini.
“Sheria
ya Takwimu No. 9 ya mwaka 2015 ni sheria inayoipa NBS jukumu la kuratibu na
kusimamia shughuli zote za upatikanaji wa takwimu rasmi nchini. Hivyo, kama
taasisi yoyote inataka kufanya utafiti kwa minajili ya kutoa takwimu rasmi ni lazima
iwasiliane na NBS ili kupata miongozo ya ukusanyaji wa takwimu rasmi,” amesema
Mangula.
Mangula
amesema kuwa, ni kosa kisheria kwa mtu yeyote ama taasisi kuendesha utafiti na
kuchapisha au kutoa takwimu rasmi bila kuwasiliana na NBS kwani inaweza
kukusanya takwimu ambazo hazina ubora na zinazoweza kupotosha umma.
Aidha,
Meneja wa Takwimu za Kodi kutoka NBS Fred Matola amesema NBS hutoa takwimu
rasmi kwa kuzingatia miongozo ya kitaifa na kimataifa inayotolewa na Umoja wa
Mataifa ili kukidhi mahitaji ya nchi pamoja na kutumika kimataifa.
“Takwimu
rasmi zinakusanywa kwa kuzingatia miongozo inayotolewa na umoja wa kimataifa ili
kukidhi mahitaji ya nchi, hivyo NBS ina wajibu kisheria kusimamia upatikanaji
wa takwimu rasmi nchini”, amesisitiza Matola.
Ofisi
ya Taifa ya Takwimu ina jukumu la kuratibu na kusimamia ukusanyaji, uchambuzi
na upatikanaji wa takwimu rasmi nchini.
...MWISHO...
Comments