PROFESA MWANDOSYA AMLILIA NDESAMBURO

Mheshimiwa Freeman Mbowe(MB), Mwenyekiti wa Taifa, CHADEMA: NIMEPOKEA KWA MASIKITIKO NA HUZUNI KUBWA TAARIFA ZA KIFO CHA MZEE WETU MHESHIMIWA PHILEMON NDESAMBURO. NILIPATA BAHATI KUFANYA KAZI NA MZEE NDESAMBURO TUKIWA WABUNGE WA BUNGE LA JAMHURY YA MUUNGANO WA TANZANIA. BINAFSI NILIFAIDIKA SANA NA MAWAZO, HEKIMA, FIKRA, NA USHAURI WAKE KATIKA MASUALA MBALI MBALI YA KIBUNGE NA KITAIFA BILA KUJALI KWAMBA TULIKUWA VYAMA TOFAUTI. 
PANDE ZOTE ZA BUNGE ZILIMTAMBUA NA KUMHESHIMU KWA UTULIVU WAKE NA HEKIMA KUBWA KATIKA KUWASILISHA HOJA ZAKE. KWA SABABU HIZO HAKIKA AMESAIDIA KATIKA KUJENGA NA KUIMARISHA DEMOKRASIA NCHINI. TAFADHALI TUFIKISHIE SALAAM ZANGU NA FAMILIA YANGU KWA FAMILIA YA MZEE NDESAMBURO NA WANA CHADEMA KWA KUMPOTEZA MUASISI NA MHIMILI WA CHAMA. KWA MWENYEZI MUNGU TULITOKA NA HAKIKA SOTE TUTARUDI KWAKE. MWENYEZI MUNGU AIREHEMU ROHO YA MAREHEMU NDESAMBURO. AMEEN.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*