Rama Mla Nyama za Watu, Baada ya Kutoka Gerezani Aanika Matukio Ya Kutisha


Mtoto aliyewahi kuwa gumzo, Ramadhan Seleman Musa aliyekuwa maarufu kwa jina la Rama Mla Watu.
DAR ES SALAAM: Exclusive! Kwa mara ya kwanza katika mahojiano maalum siku chache tangu atoke gerezani, mtoto aliyewahi kuwa gumzo, Ramadhan Seleman Musa aliyekuwa maarufu kwa jina la Rama Mla Watu ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 19, amefunguka ‘live’ juu ya mkasa wake mzima wa kunaswa akila kichwa cha mtoto.
Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally (kulia) akifanya mahojiano na Rama Mla Watu.
Kwa kumbukumbu, mwaka 2008, akiwa na umri wa miaka 11 tu, Rama alishikiliwa na vyombo vya dola nchini Tanzania kwa tuhuma za mauaji ya mtoto, Salome Yohana (3), mkazi wa Tabata jijini Dar, baada ya kukutwa na kichwa cha mtoto huyo kikivuja damu huku akikitafuna katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar, yapata miaka tisa iliyopita.
Mwaka 2013, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ilimuachia huru Rama kufuatia ripoti ya daktari iliyoonesha kuwa wakati anatenda kosa hilo alikuwa ana matatizo ya akili.
…Rama Mla Watu akiendelea kufunguka.
Tofauti na wafungwa wengine ambao wakiachiwa huru hurudi mtaani, Rama alipelekwa katika Hospitali ya Watu Wenye Matatizo ya Akili ya Mirembe mkoani Dodoma kwa kuwa ilibainika ana matatizo ya akili.
JIUNGE NA GLOBAL TV ONLINE
Katika mahojiano maalum na Global TV Online, mapema wiki hii (Jumanne iliyopita), Rama alisema kuwa, mara tu baada ya kutoka Mirembe, Dodoma takriban siku kumi na tatu zilizopita, aliamua kutembelea Global Publishers kwa kuwa ndicho chumba cha habari ambacho kilikuwa karibu naye kwa kipindi chote alichopata matatizo hayo.
KWA NINI RAMA MLA WATU?
“Jina la Rama Mla Watu nilipewa na waandishi wa habari baada ya kukamatwa na kile kichwa cha mtu. Nilikamatwa nikila kichwa cha mtoto. “Jina hilo limesababisha watu wananiogopa, watu wakiniona mtaani wanakimbia lakini ukweli ni kwamba mimi siyo yule. Kwanza nilishabadilika na nimeokoka. Watu wakigundua
ni mimi wanakimbia, siwezi kusema wananinyanyapaa bali wananiogopa.
ILIKUWAJE HADI AKAKAMATWA?
“Nilikuwa kama akili sijui imekuwaje kutokana na madawa (ushirikina). Ni kweli nilikamatwa na kichwa cha mtu. “Nakumbuka nilitoka nyumbani Segerea (Tabata, Dar) na kwenda kukitafuna pale Muhimbili na hapo ndipo nilipokamatwa.
ILKUWAJE HASA?
“Nakumbuka nilitoka zangu kucheza, nilipofika ndani (nyumbani), nilikuta kiwiliwili cha mtoto, nikawa ninajiuliza kichwa kipo wapi? Pale nyumbani nilikuwa nikiishi na mama yangu na baba wa kambo. Niliwaza sana. “Nilipoangalia vizuri nilikiona kichwa cha yule mtu kikiwa kimetundikwa kwenye mti wa mpera pale nje.
“Cha ajabu ni kwamba kile kichwa kilikuwa kinafurukuta tofauti na vingine (atafafanua kauli hii huko mbele ya simulizi), nikauliza mbona hivi? Nikaambiwa nikichukue, tukakiangalia, nikaambiwa hakina shida.
“Niliambiwa nikichukue kile kichwa nikipeleke Tegeta kwa mzee mmoja. Huyo mzee nilikuwa ninamfahamu kwa sababu alikuwa akija nyumbani na kwa wakati ule sikujua alikuwa anakwenda kufanya nini lakini alikuwa ni mtu wa madawa (mshirikina).
“Nilipotoka nyumbani, nilifika kituoni (Segerea), cha ajabu pale hakukuwa na magari mengi siku hiyo kama inavyokuwa siku nyingine. Nakumbuka kulikuwa na DCM (daladala) moja tu na sikujua lilikuwa linakwenda wapi. “Kutoka Segerea kwenda Tegeta kwa yule mzee nilitakiwa kupanda gari (daladala) tatu. Yaani kutoka Segerea hadi Ubungo kisha nishuke Mwenge halafu nichukue nyingine ya Tegeta.
“Daladala liliondoka l a k i n i lilipofika pale Ta b a t a Relini, nilishangaa likiwa linaelekea Buguruni badala ya Ubungo. Nilipouliza niliambiwa linakwenda Mnazi-Mmoja (Kariakoo).
Hapo ndipo nilipokosea masharti ya dawa niliyopewa na kukutwa na yaliyonikuta baadaye. “Nilipofika Mnazi-Mmoja, nilishuka, nikaanza kutembea na kichwa kwenye mfuko huku kikivuja damu. Nilitembea hadi Mahakama ya Samora Drive na hapo nilikuwa sielewi tena kwa sababu nilishakosea masharti ya dawa.

WATU WALIKUWA HAWAONI DAMU?
“Kutokana na dawa nilizopewa watu walikuwa hawaoni damu zilizokuwa zinachuruzika kwenye kile kichwa kwa sababu ya dawa. “Nilitembea bila kushtukiwa hadi nilipokuja kutokea Hospitali ya Muhimbili. Nakumbuka ilikuwa asubuhi. Awali niliingia vizuri tu bila kushtukiwa maana nilipewa dawa ili watu wasinione.
“Niliingia kule Muhimbili ndani nikawa nazunguka tu na kurudi getini. Niliporudi pale getini niliulizwa kwani ninakwenda wapi? Nikasema ninakwenda IPPM (Kitengo cha Huduma za Wagonjwa Binafsi) kumuona shangazi yangu aliyekuwa amelazwa, lakini nilikuwa sipaoni. “Niliendelea kuzurura kule ndani ya Muhimbili na kile kichwa hadi niliposhtukiwa baada ya kurudi pale getini na kukuta walinzi wakibadilishana zamu, walikuwa wakisainishana na kupeana sarena mabuti.
“Mmoja wa wale walinzi waliokuwa wameingia zamu alikuwa akiniangalia sana. Ndipo akaniita na kuniuliza mbona nimeloa damu? Nilikuwa nimeloa ile damu iliyokuwa inachuruzika kwenye kile kichwa kwa sababu nilikuwa ninakitafuna.
KUKITAFUNA KIVIPI?
“Nilikuwa ninakitafuna kwenye upande wa shingoni ndiyo maana ukasikia nilikuwa nikakula kichwa cha mtu na kusababisha kuloa damu.
“Baada ya kushtukiwa pale getini, yule askari aliyekuwa ananitazama sana akaniita. Nilipoona hivyo nilijua kabisa nimeshashtukiwa. Walianza kuitana wao kwa wao ili kunihoji na hapo ndipo nilipojikagua na kugundua kuwa ile dawa niliyopewa ilikuwa imeshapotea, basi akili ikawa imeshapitiwa. “Wale askari waliniuliza kwenye mfuko nilikuwa nimebeba nini? Nikawaambia kulikuwa na machungwa ninampelekea shangazi yangu pale IPPM, lakini nikawa sipaoni. “Wakaniambia mbona umeloa damu? Au umeng’atwa na mbwa? Nikawa sina majibu maana nilijua dawa ilishakwisha. “Nakumbuka hadi ninafika Muhimbili bado kile kichwa kilikuwa kinachezacheza.
Hapo ndipo nilipobanwa na wale askari kisha baadaye nilikamatwa kwa kukutwa na kile kichwa na kufikishwa mahakamani,” alisimulia Rama huku akijutia mkasa huo mbaya uliomkuta kwenye maisha yake tena akiwa na umri mdogo wa miaka 11 tu. Mkasa huu wa Rama una visa vingi vya kusisimua na kutisha juu ya maisha yake akiwa gerezani, namna alivyojihusisha na mambo ya ushirikina na kusababisha ajali za magari. Usikose wiki ijayo kwenye gazeti hilihili la Risasi Jumamosi. Ili kuona live simulizi hii tembelea Global TV Online kuanzia leo kwa kubofya www.globaltvtz. com
Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*