4x4

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU KUUZA MAHINDI NJE YA NCHI.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Na Richard Mwaikenda
SERIKALI imepiga marufuku uuzaji wa mahindi nje ya nchi na watakaokiuka watachukuliwa hatua kali ikiwemo kutaifisha mahindi na magari yanayosafirisha.

 Agizo hilo limetolewa na Wazizri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa alipokuwa akihutubia wakati wa swala ya Id el Fitri mjini Moshi leo.

Amesema wameamua kupiga marufuku usafirishaji wa mahindi nje ya nchi,  ili kulinda upungufu wa chakula nchini.

Amesema kuwa wengi wa wafanyabiashara wamekuwa wakisafirisha  vyakula kwenda nchi jirani, ili hali hapa nchini kuna uhaba wa vyakula. Ameruhusu mfanyabiashara badala ya kusafirisha mahindi asagishe na kusafirisha unga kwa kibali maalumu kutoka kwa mkuu wa mkoa.

Pia ameruhusu kusafirisha chakula kwenda mikoa yenye uhaba wa vyakula hapa nchini, badala ya kupeleka kuuza nje ya nchi.

Pia amemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, kumvua cheo askari yeyote atayejihusisha  au kuruhusu wafanyabiashara kusafirisha vyakula  nje ya nchi.
Post a Comment