SIMBA SC YASAJILI WA SITA, STRAIKA LA ZAMBIA MAWINDONI


Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
SIMBA SC imetambulisha mchezaji wa sita kusajili, ambaye ni beki Ally Shomary kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Makamu wa Rais wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amemkabidhi jezi ya klabu hiyo Shomary baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kuhamishia shughuli zake Msimbazi kutoka Manungu.
Shomary anaungana na kipa Emanuel Elias Mseja, mabeki Jamal Mwambeleko waliosajiliwa kutoka Mbao FC, Yussuf Mlipili kutoka Toto Africans zote za Mwanza, Shomary Kapombe na mshambuliaji John Bocco kutoka Azam FC. 
Makamu wa Rais wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ akimkabidhi jezi beki Shomary baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kutoka Mtibwa Sugar na chini Shomaru akisaini mkataba

Pamoja na hayo, tayari kuna taarifa Simba SC imemsajili kipa namba moja Tanzania, Aishi Manula, huku pia ikiwa mbioni kumrejesha mshambuliaji wake wa zamani, Mganda Emmanuel Okwi kutoka SC Villa ya kwao.
Mshambuliaji wa FC Nkana ya Zambia, Walter Bwalya naye anatajwa kuwa kwenye rada za Wekundu wa Msimbazi.
Simba inafanya usajili wa kishindo, baada ya kufanikiwa kukata tiketi ya kurejea kwenye michuano ya Afrika mwakani kwa mara ya kwanza baada ya mitano.
Wekundu hao wa Msimbazi watashiriki Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, kufuatia kutwaa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) mei 27 mwaka huu kwa kuifunga Mbao FC 2-1 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma. 

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA