SIMBA WA KIMATAIFA YATOLEWA SPORTPESA SUPER CUP

Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
SIMBA SC imeaga mapema michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kufungwa kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 0-0 na Nakuru All Stars ya Kenya jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog hakukaa hata mara moja kipindi cha pili, akiiongoza timu yake kwa kuwalekeza wachezaji wake cha kufanya ili kupata ushindi, lakini haikusaidia na mchezo ukaisha 0-0.
Kipa Mghana, Daniel Agyei akakosa penalti ya pili ya Simba na mikwaju yote ya wachezaji wa Nakuru ikampita, Simba ikilala 5-4 na kuungana na Singida United, Tusker ya Kenya na Jang’ombe Boys kuaga mashindano mapema.
Waliofunga penalti za Nakuru All Stars, timu ya Daraja la Kwanza Kenya ni Baraka Nturukundo, Aman Kyata, Maina Kangethe, Amakanji Ekmba na Kamau Nganga, wakati za Simba zilifungwa na janvier Besala Bokungu, Mwinyi Kazimoto, Hafidh Mussa na Fiston Munezero.  
Mshambuliaji Juma Luizio anayecheza kwa mkopo kutoka Zesco United ya Zambia alianza kipindi cha kwanza, lakini akashindwa kuipenya ngome ya Nakuru All Stars iliyoongozwa na beki Mtanzania mwenzake, Amani Kyata aliyewahi kuchezea African Lyon.
Kipindi cha pili akaongezewa nguvu ya mshambuliaji Muivory Coast, Frederick Blagnon ambaye hakika alikwenda kuisumbua ngome ya timu ya Nakuru, lakini hawakuweza kufunga hata bao la kuotea.
Nakuru sasa itamenyana na Gor Mahia Alhamisi, wakati Nusu Fainali nyingine itazikutanisha bingwa wa Tanzania, Yanga na AFC Leopards ya Kenya. Yanga iliwatupa nje mabingwa wa Kenya, Tusker wakati Leopards iliitoa Singida United na Gor Mahia imeitoa Jang’ombe Boys ya Zanzibar kwa mabao 2-0.   
Kikosi cha Simba kilikuwa; Daniel Agyei, Janvier Bokungu, Jamal Mwambeleko, Mwinyi Kazimoto, Feston Munezero, Yussuf Mlipili, Bakari Masoud, Jamal Mnyate/Frederick Blagnon dk46, Juma Luizio, Pastory Athanas na Mohammed Ibrahim.
Nakuru All Stars: Martin Lule, Kamau Nganga, Sadick Wainaina, Sadicky Mukhwana, Amakanji Ekmba, Siwa Omondi/Nturukundo Baraka dk70, Amani Kyata, Ng'ang'a Anthony, Nandwa Sosi, Maina Kangethe na Kamau Ndungu.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

KWA HERI KAMANDA WETU ABBAS KANDORO

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA

YANGA SC WAANZA KAZI AFRIKA LEO…WANAKIPIGA NA U.S.M. ALGER SAA 4:00 USIKU ALGERIA

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.