SINGIDA UNITED YATOLEWA MAPEMA SPORTPESA SUPER CUP


Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM 
TIMU ya AFC Leopard ‘Ingwe’ imekuwa ya kwanza kwenda Nusu Fainali ya SportPesa Super Cup baada ya ushindi wa penalti 5-4 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.
Beki Salum Chukwu aliyesajiliwa kutoka Toto Africans alifanya kazi nzuri ya kuwadhibiti washambuliaji wa Ingwe, lakini akaenda kupiga juu ya lango mkwaju wake wa penalti.
Waliotumbukiza kambani matuta ya AFC Leopard ni Bernard Mangoli, Marselas Ingotsi, Kateregga Allan, Duncan Otieno na Fiamenyo Gilbert, wakati za Singida zilifungwa na Atupele Green, Hamisi Shengo, Nhivi Simbarashe na Muroiwa Elisha.
Kocha wa Singida United, Mholanzi Hans van der Pluijm akifuatilia mchezo leo 
Hamisi Shengo wa Singida United (kulia) akijaribu kumpita beki wa AFC Leopards, Michael Kibwage 

Singida United inayofundishwa na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 20 kupitia kwa Mzimbabwe Kutinyu Tafadzwa, kabla ya Ingwe kusawazisha kupitia kwa Vincent Oburu dakika ya 63.
Baada ya hapo, timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu na kosa kosa za pande zote mbili hadi mchezio kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti.
Kwa matokeo hayo, AFC Leopard atakutana na mshindi kati ya Yanga na Tusker ya Kenya pia zinazomenyana muda huu katika mchezo wa michuano hiyo.
Kikosi cha Singida United kilikuwa; Lubawa Said, Muroiwa Elisha, Msonjo Roland, Dumba Hassan, Chukwu Salum, Ally Kenny, Mtasa Wisdom, Kutinyu Tafadzwa/ Kagoma Yussuf dk85, Green Atupele, Nhivi Simbarashe/ Nizar Khalfan dk 75 na Shengo Hamisi.
AFC Leopards; Gabriel Andika, Dennis Sikhai, Marcus Abwao, Abdallah Salim, Duncan Otieno, Isuza Whyvonne, Mangoli Bernard, Joshua Mawira, Fiamenyo Gilbert, Haron Nyakha/Allan Kateregga dk63 na Vincent Oburu.

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NAMAINGO YAZINDUA HEKA 7000 ZA MASHAMBA MJI KIJIJI CHA MSOLWA, MKURANGA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

HABARI MPASUKOOO:GARI LAGONGA WATOTO KUIKWEPA BODABODA GONGO LA MBOTO

HARAMBEE YA UJENZI HOSPITALI YA MUHEZA YAVUKA MALENGO, ZAPATIKA BIL. 1.6

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

WAZIRI SHONZA AMJIBU DIAMOND

HABARI MPASUKOOO!!! MCHAWI ADONDOKA AKIWA UCHI KIVULE,DAR

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI