SPORTPESA; UJIO WA EVERTON KUUTANGAZA UTALII WA TANZANIA KIMATAIFA

 Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya SportPesa, Abbas Tarimba akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, kuhusu ujio wa timu ya Ligi Kuu ya England ya Everton ambayo itacheza na Gol Mahia kwenye Uwanja wa Taifa Julai 13, mwaka huu. Kulia ni Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania, Geofrey Meena.Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa SportPesa,Pavel Slavkov,HABARI, PICHA NA RICHARD MWAIKENDA

KLABU ya Everton ya Uingereza, inatarajia kutembelea vivutio vya kitalii nchini itakapokuja mwezi ujao kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya. 

Mchezo huo unatarajiwa kucheza saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo Gor Mahia ilipata nafasi hiyo baada ya kuibuka bingwa wa mashindano ya SportiPesa Super Cup. Akizungumza Dar es Salaam jana, 

Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya SportiPesa, Tarimba Abassi alisema ujio wa Everton  nchini utaleta manufaa makubwa ikiwemo kuitangaza Tanzania katika nchi nyingine duniani sehemu mbalimbali za utalii hapa nchini. “

Leo tumefungua rasmi ujio wa Everton hapa nchini na ujio huu unafaida kubwa moja ni kuitangaza Tanzana katika Ligi ya Uingereza ambapo watavaa jezi zenye nemba itakayo andikwa VISIT TANZANIA ambayo tunaimani tutapata watalii wengi katika nchini yetu,” alisema na kuongeza; “

Ujio huu utaitangaza nchi yetu Dunia nzima na kuifanya Tanzania kuendelea kuaminika kwa nchi zingine na kuweka shauku ya timu za nchi nyingine kuweza kuja kucheza na timu za hapa nyumbani”

 Kwa upande wa Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi alisema anaishukuru kampuni hiyo katika kuendeleza soka hapa nchini. 

“Kama shirikisho tunawaheshimu wawekezaji wanaokuja kuwekeza katika soka hapa nchi, zamani tulikuwa tunacheza mpira kama kujifurahisha lakini kwa sasa mpira ni ajira, hivyo wazazi wawaendeleze watoto wao wenye vipaji kwa sababu kutakuwa na mafunzo kwa vijana wa Tanzania watakaofundishwa na timu ya everton,” alisema. 

Everton itawasili nchini Julai 12, mwaka huu kwaajili ya mechi hiuo ya kirafiki. Tarimba akifafanua jambo wakati wa mkutano huo
 Mkurugenzi wa Ufundi wa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi (katikati) akielezea semina mbalimbali zilizoandaliwa na shirikisho hilo wakati wa ujio wa Everton nchini Julai 12, mwaka huu. Zitakuwepo semina kwa makocha, waamuzi na waandishi wa habari za michezo.
 Baadhi ya wanahabari wakiwa katika semina hiyo iliyofanyika leo kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, Dar es Salaam

 Meneja Masoko wa TTB, Geofrey Meena akielezea faida mbalimbali ambazo Tanzania itapata kutokana na ujio wa timu ya Everton nchini ambapo alisema kuwa utalii wa Tanzania utatangazika sana duniani, pia fursa za uwekezaji zitaongezeka nchini na hata bishara itakuwa.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa  na Michezo, AlexMkeyenge, akielezea jinsi Serikali ilivyojianzaa kuipokea timu hiyo pamoja na maandalizi mazuri ya uwanja wa Taifa patakapofanyika mechi Julai 13, mwaka huu.

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA

DC MKURANGA AZINDUA MRADI WA MASHAMBA MJI YA NAMAINGO MSOLWA

TGGA WAMUAGA BOSS WA GIRL GUIDES AFRIKA KWA HAFLA KABAMBE

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

Wasafi TV kuanza kurusha matangazo yake leo (+video)

WAGGGS AFRIKA WAIPONGEZA TGGA KWA KUONGOZA AFRIKA KUSAJILI GIRL GUIDES WENGI