4x4

Staa David Beckham ndani ya Mbuga ya Serengeti


Siku chache zilizopita Legend wa soka wa England David Beckham aliripotiwa kutua Tanzania kimya kimya baada kusambaa video fupi ikimuonesha akiwa Julius Nyerere International Airport  Dar es Salaam pamoja na familia.
New story iliyonifikia ni kwamba Beckham ambaye ni staa wa zamani wa Manchester United, Real Madrid na England amekuja Tanzania kwa ajili ya mapumziko ambapo atatembelea vivutio mbalimbali vya Utalii na hapa ninazo baadhi ya picha zikimuonyesha akiwa na familia yake kwenye Mbuga ya Serengeti.
Mbali na Beckham, mastaa wengine walioekana kutembelea Mbuga za Wanyama Tanzania mwaka huu ni pamoja na Will Smith na Mwanamitindo Chanel Iman ambao walifika Serengeti March 2017.
David Beckham na mwanae Brooklin
Beckham pia alitumia ukurasa wake wa Instagram David Beckham kusifia uzuri wa mbuga hiyo>>>

Post a Comment