STAR TIMES KUONESHA KOMBE LA MABARA

Abraham Ntambara
KAMPUNI ya StarTimes imesema itaonyesha michuano ya Kombe la Mabara yanayotarajia kuanza Juni 17 hadi Julai 2 mwa ka huu nchini Urusi.
Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Ofisa Uhusiano wa Kampuni hiyo Josephine Stephen, alisema mashindano hayo yatatumika kama maandalizi ya mashindano ya kombe la dunia yatakayofanyika mwakani.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ilisema mashindano haya yatakuwa ya kiwango cha juu ambapo mabingwa wa kombe la dunia Ujerumani wanatarajia kupeleka timu yenye wachezaji vijana, hivyo nchi nyingine zinaona kama ni fursa ya pekee.
Aidha ilisema kuwa nchi ya Ureno ambayo ni mabingwa wa kombe la Ulaya watakuwa ikiongozwa na mchezaji wao nyota Christian Ronaldo ambapo inataka kuweka historia katika mashindano hayo.
Lakini pia katika michano hiyo Arturo Vidal na timu yake ya Chile ambao pia ni washiriki katika fainali hizo hawatatamani kuondoka watupu.
Taarifa ilifafanua kundi B, litakuwa  na timu ya Chile ambayo ndiyo inapewa nafasi kubwa ya kuongoaza kundi hilo, lakini vijana wa Ujerumani watataka kuwaonyesha kaka zao kuwa wako tayari kuchukua nafasi zao katika timu ya Taifa huku timu ya Cameroon mabingwa wa Bara la Afrika wakiwa na matarajio madogo pamoja na timu ya Australia.
Kundi A, litakuwa na timu za New Zealand, Ureno, Mexco na mwenyeji Ureno ambayo itanufaika na uwepo wa mashabiki wake.
“Swali la uhakika ni kwamba: Je mshindi atavunja mwiko wa wa kombe hili la Mabara? Tangu kuanzishwa mashindano haya hakuna bingwa wa kombe hili aliyewahi kuwa mshindi wa kombe la dunia. Mfano Brazil alishinda kombe hili mara tatu lakini hakufanikiwa katika mashindano ya kombe la dunia yaliyofuata,” alisema Ofisa Uhusiano na Meneja Masoko wa StarTimes Tanzania Juma Suluhu.
StarTimes kama mshirika rasmi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) itaonyesha mashindano hayo kupitia chaneli zake zote za michezo pamoja na channeli za ICC na DFL Supercup.
Aidha licha ya kuonyesha michuano hiyo itatoa ofa maalumu katika kipindi cha msimu wa sabasaba za tamthilia pamoja na program za watoto.

mwisho
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

KWA HERI KAMANDA WETU ABBAS KANDORO

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.

YANGA SC WAANZA KAZI AFRIKA LEO…WANAKIPIGA NA U.S.M. ALGER SAA 4:00 USIKU ALGERIA

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA