TAZAMA MAZIKO YA MKE MDOGO WA MZEE YUSUF


Marehemu Chiku aliyefariki jana katika Hospitali ya Amana jijini Dar
Waombolezaji na ndugu wakilisawazisha kaburi la marehemu Chiku aliyefariki jana katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam wakati akijifungua. Mtoto wake pia aliyekuwa tumboni alifariki.
Mzee Yusufu akiongoza waombolezaji kumwombea dua marehemu mkewe, Chiku.
Mzee Yusuf (wa kwanza kushoto) akiingia kaburini kuupokea mwili wa mkewe, Chiku.
Maziko yakiendelea.
Mzee Yusuf akiwa katika masikitiko makubwa.
Waombolezaji mbalimbali waliofika katika mazishi hayo.
 
Jeneza la mwili wa marehemu likiingizwa katika makaburi ya Kisutu mchana wa leo.
Mzee Yusufu akiwa amebeba mwili wa mtoto wake aliyefariki.
Safari ya kuelekea makaburi ya Kisutu ikianzia nyumbani kwa marehemu.
Mmoja wa waombolezaji akisoma kaswida.
Mzee Yusuf akisaidiwa kuingia katika makaburi ya Kisutu.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo (katikati) wakati wa mazishi. Kushoto ni Meneja wa Ukumbi wa Burudani wa Dar Live, Juma Mbizo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo akisalimiana na Mzee Yusuf.
MAMIA ya waombolezaji leo wamemzika marehemu Chiku Hamisi aliyekuwa mke wa mwimbaji taarab aliyestaafu na kumrudia Muumba wake, Ustaadhi Mzee Yusuf.  Chiku aliyezikwa kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar leo mchana, alifariki dunia katika Hospitali ya Amana jijini Dar Jumamosi  jioni ambapo alikwenda kujifungua.
Chiku alipoteza maisha akisaidiwa na wauguzi kujifungua kwa njia ya upasuaji ambapo  mwanaye aliyekuwa tumboni alifariki pia.
Shughuli za msiba na mazishi zilianzia nyumbani hapo Kariakoo Mtaa wa Amani na Livingstone ambapo mwili  ulitolewa nyumbani hapo na kwenda kuswaliwa kwenye msikiti wa Manyema.
Baada ya suala mwili ulipelekwa makaburi ya Kisutu jijini hapa.
Katika mazishi hayo Mzee Yusuf alishindwa kuzungumza chochote baada ya kuishiwa nguvu ambapo aliondolewa makaburini hapo kwa msaada wa waombolezaji.

Na Richard Bukos/GPL
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NDANI YA CHAKE CHAKE,MKOA WA KUSINI PEMBA LEO.

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.