TUPATE MANENO YA BUSARA KIDOGO TOKA KWA WATU MAARUFU DUNIAN


1. "Ni afadhali kuwa na jeshi la kondoo linaloongozwa na Simba, kuliko jeshi la simba linaloongozwa na kondoo."
# Napoleon_Bonaparte .
2. "Lengo la kwanza la vita sio kufa kwa ajili ya nchi yako, hapana. Bali ni kuua mtu mwingine kwa ajili ya nchi yake."
# George_Patton .
3. "Lazima nisome siasa na vita ili mwanangu apate uhuru wa kusoma hesabu na falsafa." # John_Adams .
4. "Washindi wanashinda kwanza halafu wanakwenda vitani, wanaoshindwa huenda vitani kwanza halafu ndio wanatafuta ushindi." # Sun_Tzu .
5." Maisha ni mfululizo wa matatizo Na chembechembe ndogo za raha, ukiwa Na raha au shida mda wote jua hayo siyo maisha" Kevin Nathan Tanzania
6. "Inafahamika vizuri katika vita, majeruhi wa kwanza ni ukweli. Kwamba, wakati wa vita, ukweli huharibiwa vibaya na propaganda." # Harry_Browne .
7. "Propaganda ikitumiwa vizuri inaweza kumfanya mtu aone kuwa paradiso ndio jehanam na jehanam ndio paradiso."
# Adolf_Hitler .
8. "Mtu mwenye ufahamu wa kweli, si tu kwamba atawapenda maadui zake wanapofanya vizuri, bali pia atawachukia marafiki zake wanapokosea."
# Friedrich_Nietzsche
9. "Madaraka ni kama mchanga. Jinsi unavyoyakumbatia kiganjani ndivyo yanavyokuponyoka." # Confucus
10. "Tofauti kati ya akili na ujinga ni kuwa, akili ina kikomo, ujinga hauna kikomo."
# Albert_Einstein .
11." Tanzania ni nchi pekee ambayo wanachama wa chama tawala ufurahia wapinzani kuteswa ,Na kusahau kuwa ipo siku wanaweza kuwa wapinzani wakateswa pia" Mulisa Kiberenge , Tanzania,
12. "Kuna watu wawili tu wasioweza kubadili mawazo. Mpumbavu kuliko wote na mwenye hekima kuliko wote." # Plato.
13. "Rais ni mtu wa kushutumiwa kila mara. Ukiona hataki kushutumiwa, ujue hajui sababu ya kuwa hapo."
# Harry_Truman
14. "Sote tumezaliwa wajinga, tunahitaji juhudi kidogo ili kuwa na maarifa, au bidii kubwa sana ili kuendelea kubaki wapumbavu. Baadhi huchagua njia ya pili." # Benjamin_Franklin
15. "Nchi za ulimwengu wa tatu ni nchi pekee ambazo wapinzani hufurahia mipango ya serikali kufeli wapate cha kuhongea kwa wananchi badala ya kushirikiana Na serikali kuleta maendeleo" Kevin Issaya NPP
16"Unajisi wa sheria hutokea pale ambapo mahakmu/majaji, hujiweka mikononi mwa watawala na kuamini watawala wana nguvu kuliko sheria"
# Lamar_Smith
17. "Kuliko kuwapa wanasiasa ufunguo wa maisha yako, ni bora ubadili kitasa"
# Doug_Lar
Je umependa ipi?? Comment namba ya point ulopenda
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)