UJUE WASIFU BABKUBWA WA PROFESA MWANDOSYA

 PROFESA MARK MWANDOSYA
Kwa hakika kabisa. Cv hii imeshiba. Nimefurahishwa na WASIFU na MAELEZO BINAFSI YA PROFESA M. J. MWANDOSYA, naamua kumpatia heshima kubwa ya uwezo alionao kielimu na Mungu ambariki sana.
A: Binafsi
Jina: MWANDOSYA, Mark James
Tarehe ya Kuzaliwa: 28 Desemba, 1949
Mahali pa kuzaliwa: Mbeya
Maelezo ya Familia: Nimeoa na tuna watoto watatu na wajukuu wawili.
B: Elimu
Elimu ya Msingi:
Shule ya Msingi Majengo, Mbeya, 1957 – 1958
Shule ya Msingi Chunya, 1959 – 1960
Shule ya Kati Chunya, 1961 – 1964
Elimu ya Sekondari:
Shule ya Sekondari Malangali, 1965 – 1968
Chuo vcha Ufundi Dar es Salaam, 1969 - 1970
Elimu ya Juu:
Chuo Kikuu cha Aston, Uingereza, 1971-1974
Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza, 1974-1977
Shahada:
Shahada ya Uhandisi Umeme ya Chuo Kikuu cha
Aston (Bachelor of Science 1st Class Honours,
University of Aston), 1974
Shahada ya Udaktari wa Falsafa ya Chuo Kikuu cha
Birmingham (Doctor of Philosophy in Electronic and
Electrical Engineering, University of Birmingham),
1977
C: Uzoefu katika kazi na Uongozi
i. Kazi:
1. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) 2012
2. Mkuu (Chancellor), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (Mbeya
University of Science and Technology-MUST) (2014-mpaka sasa)
3. Waziri wa Maji (2010-2012)
4. Waziri wa Maji na Umwagiliaji (2008-2010)
5. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) (2006-2008)
6. Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi (2000-2005)
7. Mbunge wa Rungwe Mashariki (2000 – 2015)
8. Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi
(2002 – mpaka sasa)
9. Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara, (1992-1993)
10. Katibu Mkuu, Wizara ya Maji, Nishati na Madini, (1990-1992)
11. Kamishna wa Nishati na Petroli, Wizara ya Nishati na Madini (1985-1990)
12. Mkurugenzi, Kituo cha Nishati, Mazingira, Sayansi na Teknolojia (CEEST),
(1993-2000)
13. Profesa wa Uhandisi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (1987-2000)
14. Profesa Mshiriki wa Uhandisi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1983-1987)
15. Mtafiti (Sayansi), Chuo Kikuu cha Princeton, Marekeni, (1983-1984)
16. Mhadhiri Mwandamizi (Uhandisi Umeme), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(1980- 1983)
17. Mhadhiri (Uhandisi Umeme), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1977-1980)
18. Mhandisi, Kampuni ya General Electric Company, Manchester, Uingereza, (1977-
1978)
19. Mhadhiri Msaidizi (Uhandisi Umeme), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (1976-
1977)
ii. Uongozi:
1. Mjumbe, Bodi ya Usimamizi wa Jopo la UNEP la Kimataifa la Matumizi Bora ya
Rasilimali (UNEP International Resource Panel).
2. Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia
(TAZARA) Nyakati tofauti,( 2000-2005)
3. Mwenyekiti, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, (1996-2000)
4. Mwenyekiti, Kituo cha Nishati, Mazingira, Sayansi na Teknolojia, (1993-2000)
5. Mwenyekiti, Kampuni ya Siemens (Tanzania) Ltd, (1999-2000)
6. Mwenyekiti, Kampuni ya Kibo Paper Industries Ltd, (1995-1998)
7. Mwenyekiti, Kampuni ya Williamson Diamond Company Ltd, (1990-1992)
8. Mwenyekiti, Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda, (Tanzania Industrial
Research and Development Organisation), (1994-1998)
9. Mwenyekiti, Tanzanian and Italian Petroleum Refinery (TIPER), (1987-1993)
10. Mwenyekiti, Mamlaka ya Maji Mijini (NUWA), (1991-1993)
11. Mwenyekiti, Bodi ya Utawala ya Chuo cha Biashara, (1992-1993)
12. Mwenyekiti, Kampuni ya Gesi (GASCO), (1998 -2000)
13. Mwenyekiti, Kamati ya kutayarisha Sera ya Nishati, (1988-1991)
14. Mwenyekiti wa Kundi la nchi zinazoendelea (G77) na Msemaji Mkuu wa nchi
hizo na China katika majadiliano ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani yailyo
fanikisha kupatikana kwa Itifaki ya Kyoto,(1997)
15. Mwenyekiti, Timu iliyoandaa Itifaki ya Sekta ya Nishati ya Jumuiya ya
Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)
16. Makamu Mwenyekiti, Tume ya Taifa ya UNESCO, (1983-1988)
17. Makamu Mwenyekiti, Shirika la Maendeleo ya Taifa, (National Development
Corporation-NDC), (1992-1993)
18. Makamu Mwenyekiti, Bodi ya Wadhamini, Southern African Development
through Electricity (SADELEC) ya Afrika ya Kusini, (1994-1998)
19. Kamishna, Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirkia ya Umma, (1996-1999)
20. Kamishna, Tume ya Mawasiliano, (1999-2000)
21. Mkurugenzi, TAZAMA Pipeline Lted, (1987-1993)
22. Mkurugenzi, National Textile Corporation TEXCO, (1993)
23. Mkurugenzi, Tanzania Zambia Railway Authority TAZARA, (1992-1993)
24. Mkurugenzi, Shirika la Posta na Simu, TPTC, (1981-1986)
25. Mkurugenzi, Shirika la Ugavi wa Umeme, Tanesco, (1985-1990)
26. Mkurugenzi, Shirika la Maendeleo ya Petroli, TPDC, (1985-1990)
27. Mkurugenzi, Kilwa Ammonia Company Ltd (KILAMCO), (1985-1990)
28. Mkurugenzi, Standard Chartered Bank Tanzania Ltd, (1999-2000)
29. Mkurugenzi, AGIP (Tanzania) Ltd, (1989-1991)
30. Mjumbe, Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (1994-2000)
31. Mjumbe, Baraza la Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (1994-2000)
32. Mjumbe, Baraza la Utawala IDM-Mzumbe, (1992-1993)
33. Mjumbe, Baraza la Utafiti wa Kisayansi (Tanzania National Scientific Research
Council), (1981-1983)
34. Mjumbe, Kamisheni ya Sayansi na Teknolojia, (Tanzania Commission for Science
and Technology), (1987-1990)
35. Mjumbe, Timu ya kuandaa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025.
36. Mjumbe, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, (National
Environment Management Councli-NEMC), (1999-2000)
iii. Uwakilishi wa Nchi katika Mikutano ya Kimataifa
1. Mkutano Mkuu wa 20 wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO), Paris, France, Novemba, 1978
2. Mkutano Mkuu wa 21 wa UNESCO, Belgrade, Yugoslavia, Oktoba 1980
3. Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu nishati mpya ya Nishati Mbadala,
Nairobi, Kenya Agosti, 1981.
4. Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Nishati Mbadala, Rome, Italia, June 1982
5. Mkutano Mkuu (wa 4 wa dharura) wa UNESCO, Paris, Novemba, 1981
6. Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Nishati Mbadala, New York, Mei, 1984
7. Mkutano wa UNESCO wa Mawaziri wa Afrika wa Sayansi na Teknolojia,
Arusha, Julai, 1987
8. Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa,
Berlin, Ujerumani, Aprili, 1995
9. Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa,
Geneva, Uswisi, Desemba, 1996
10. Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa,
Kyoto, Japan, Novemba, 1997.
11. Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa
Buenos Aires, Argentina, Oktoba, 1998
12. Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa,
Bonn, Ujerumani, Oktoba, 1999
13. Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya Hali ya Hewa,
Bali, Indonesia 2009
14. Mikutano ya Maafisa na ya Mawaziri wa Nishati na Madini katika Jumuiya ya
Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, (SADC), 1985-1992
15. Mikutano ya Maafisa na ya Mawaziri wa Biashara na Viwanda ya Jumuiya ya
Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, 1993
16. Mikutano ya Maafsia na ya Mawaziri wa Biashara na Viwanda ya Preferential
Trade Area (sasa COMESA), 1993.
17. Nimeongoza ujumbe wa Tanzania katika majadiliano na Benki ya Dunia (World
Bank) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (African Development Bank (AfDB)
kuhusu mikopo nafuu kuendeleza na kuboresha usambazaji wa umeme na
petroli, 1988-1992
18. Nimeongoza ujumbe wa Tanzania katika mikutano mbalimbali ya Kimataifa
inayohusu usafiri wa anga, maendeleo ya simu duniani, bandari, maendeleo ya
reli, mazingira, maji na umwagiliaji.
19. Nimehudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Mataifa kuhusu
Habari na Mawasiliano, Geneva, Uswisi, Desemba 2003 nikimwakilisha Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
20. Mkutano Mkuu wa Shirika la Biashara (WTO), Hong Kong, 2005.
D: Ushauri (Consultancy)
i. Nimetoa ushauri wa kitaalam kwa vipindi mbalimbali kwa Serikali za nchi
zifuatazo: Nambia, Zimbabwe, Eritrea
ii. Nimetoa ushauri wa kitaalam kwa mashirika ya Kimataifa yafuatayo: UNDP,
UNEP, UNESCO, GTZ, USCSP, GEF, SADC, OAU, UNECA
iii. Niliongoza timu ya wataalam tulioandaa Itifaki ya Ushirkiano katika Nishati
katika nchi za SADC
iv. Niliandaa rasimu ya kwanza ya Mkataba wa ushirikiano katika Nishati na
Maliasili wa Umoja wa Nchi za Kiafrika (OAU)
E: Uzoefu katika Siasa
1. Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (2002 – mpaka
sasa)
2. Mwanachama wa CCM (1977 mpaka sasa)
3. Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la Umoja wa Vijana wa CCM Ofisi
Ndogo ya Makao Mkuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, (2000 -2005)
4. Naibu Kamanda, Vijana wa CCM Wilaya ya Rungwe (1998 mpaka Machi 2000)
5. Mwanachama wa TANU (1971-1977)
6. Mwanachama, Umoja wa Vijana wa TANU (1967-1971)
7. Mwanachama, Umoja wa Vijana wa TANU (1967-1971)
8. Makamu wa Mwenyekiti Umoja wa Vijana wa TANU, Tawi la Shule ya
Sekondari ya Malangali, (1967-1968)
9. Mwenyekiti Umoja wa Wanafunzi wa Afrika, Chuo Kikuu cha Birmingham,
1975
F: Mada, Maandishi, na Vitabu
1. Mada: Nimeandika na kuchapisha mada 36 katika majarida ya kitaalamu nchini
na nchi za nje.
2. Ripoti za Utaifiti: Ripoti 12 za utafiti mbalimbali zimechapishwa ndani na nje ya
nchi.
3. Uhariri: nimehariri majarida na vitabu 9
4. Vitabu: nimeandika vitabu 10 katika uhandisi, nishati, mazingira na maendeleo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*