Upendo, Furaha na Amani ya Ramadhani Endelea Nayo!

NIANZE kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa wema wake, kwa kunivusha kwenye changamoto nyingi ambazo nakutananazo. Pili nikutakie heri ya Sikukuu ya Idd msomaji wa Magazeti ya Global Publishers na safu hii ya XXLove.

Mfungo wa Ramadhani, umeisha, walio Waislam na wasiyo wamejifunza kitu, wamejifunza kuhusu toba ya kweli kuwa ni kufunga na kuomba.
Hata mtu mmojammoja ambaye yuko kwenye ndoa au uchumba, kuna jambo kubwa sana amejifunza, sasa hebu jaribu kutumia uzoefu ulioupata wakati wa mfungo kwenye maisha yako ya kila siku.

Endelea kuonesha upendo kwa mwenza wako kama ilivyokuwa kwenye Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Jitahidi kurudi na kuwasiliana na mwenza wako kwa ukaribu zaidi kama ambavyo ulikuwa unawasiliana naye katika kuomba na kutoa fedha ya kuandalia futari.
Bado ninaendelea kusisitizia kuhusu kudumisha upendo, furaha na amani ambayo wewe msomaji uliidumisha kipindi chote ulichokuwa kwenye Mwenzi Mtukufu wa Ramadhani. Hata kama ulikuwa hujafunga kwa sababu hukutaka kufunga au hukufunga kwa sababu maalum, lakini ninaamini ulifanya toba kwa namna yoyote ile.

Ninaamini mambo mengine kwenye uhusiano au ndoa yako yalienda sawia. Mwenye mke aliyekuwa anasumbua, basi alikuwa tuli akifanya toba yake. Mwanaume aliyekuwa karaha kwa mkewe, basi alibadilika na kutengeneza furaha kwa mkewe, aliungana naye katika kutimiza majukumu ya familia yake.

Wazazi waliokuwa wakiishi kwa mazoea ya kuchelewa kurudi nyumbani kwa ajili ya kujumuika na watoto wao, basi nao walijitahidi kuwahi.
Kama kila mtu atatumia upendo, furaha na amani ileile aliyoitumia kipindi cha mfungo, basi mapenzi na uhusiano wako vitadumu na mambo yatakuwa mazuri siku zote, kwa sababu kila mtu ana hofu ya Mungu. Kila mtu anatamani kuendelea kuwa msafi katika maisha ya ndoa au uhusiano wake.

Siku zote mapenzi yanahitaji ukarimu, upendo na furaha ya moyo zaidi ya chochote, basi endelea kutumia toba yako ili kukufanya uwe na amani kwa mwenza wako na familia yako. Kama ukiwa na amani basi furaha huja moja kwa moja miongoni mwenu.
Huna budi kuishi kwa kufuata na kutimiza matakwa ya Mungu ili kukupunguzia machungu ya maisha, mateso ya ndoa yako au unafuu, urahisi na utashi wa kumpata mchumba mwema atakayekufaa.

Ukiweza kuishi kwa kufuata misingi na taratibu ambazo uliziishi katika mwezi mtukufu, basi ndoa yako haitakuwa na makelele, mapigano wala mabishano. Uliye kwenye uchumba utafanikiwa hadi utafikia ndoa yako, kwani Mwenyezi Mungu atakuwa anakusimamia kwa sababu unamtii na kumuishi.
Kwa maoni na ushauri, tembelea ukurasa wetu wa Gazeti la Ijumaa Wikienda kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook.

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA