VIONGOZI WA DINI WAOMBWA KUSAIDIA KUFICHUA WANAOJIHUSISHA NA MAUAJI KIBITI

Abraham Ntambara
VIONGOZI wa Dini wameombwa kusimama mstari wa mbele katika kuhakikisha wanaisaidia serikali kwa kuhamasisha ili kuendelea kufichua na kuwabaini wahalifu wanaendelea kujihusisha na mauaji ya Kibiti, Mkoani Pwani na maeneo mengine.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mchungaji wa Mitume, Manabii na Maaskofu Tanzania Komando Mashimo wa Huduma ya Njili ya Maumivu na Uponyaji wakati akizungumza na vyombo vya habari, alisema suala hilo la mauaji halivumiliki.

Aidha alibainisha kuwa lengo la kuomba  viongozi wa dini kufanya hivyo nikutokana na wao ndiyo waliobeba watu wengi katika Makanisa na Misikiti ambao ni rahisi kwao kuwahamasisha na kuweza kutoa ushirikiano.

Alieleza kuwa kila kukicha watu wasio na hatia wamekuwa wakiuawa huku viongozi wa hao wakishindwa kutilia mkazo katika kulitafutia ufumbuzi wa suala hilo kwa kuisaidia serikali.

“Naomba viongozi wa dini wasimame kwa pamoja wahamasishe makanisani mwao, tuilinde amani na kila mtanzania awe mlinzi juu ya mwenzake, akimuona mwenzake anafanya mambo yasiyo faa, basi atoe taarifa kwenye vyombo husika ili hatua ichukuliwe,” alisema Mashimo.

Aidha alisema Tanzania ina Manabii 988 ambapo alitoa rai kwa manabii hao kusimama na kueleza walipojificha waharifu hao kwani wao husimama kama siko la Taifa.
Alifafanua kuwa kazi ya nabii ni kutoa maelekezo ambapo alisema kuwa waache kutoa tu maji ya upako na badala yake wajikite pia katika kulisaidia Taifa katika kutatua tatizo hilo la mauaji.

“Manabii watuambie watu hawa wako wapi, wamejificha sehemu gani , kama kweli Mungu anawatumia watuambie kwani kazi yao ni kuilinda nchi na kufichua yaliyofichika,” alisema.
mwisho


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.