WANYAMA AMTABILIA MAKUBWA SAMATTA

Mwandishi wetu
KIUNGO wa timu ya Taifa ya Kenya (Harambee Stars) na Klabu ya Tottenham ya England, Victor Wanyama (pichani), ametua nchini kuja kupumzika huku akimtabiria makubwa Mtanzania, Mbwana Samatta katika soka la kimataifa. Wanyama aliwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam baada ya kuiwezesha klabu yake kumaliza kwa kushika nafasi pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya England nyuma ya mabingwa Chelsea. Kwa mujibu wa mahojiano ya Wanyama na Blogu ya Shafiidauda, si mara mara ya kwanza kufika Tanzania lakini kipindi hiki amekuja maalumu kwa ajili ya kupumzika na kuifahamu nchi kwa ujumla wake. “Nilikuwa ni mtu wa kuingia na kutoka, lakini hivi sasa nitakuwa hapa nchini kwa muda mrefu na nadhani nitajua vitu vingi,” alisema Wanyama. Mbali na hilo, alipoulizwa kuhusu soka la Tanzania na jinsi anavyomfahamu Samatta ambaye anacheza soka la kulipwa Ubelgiji katika timu ya KRC Genk, alijibu:” Soka la hapa nalijua na timu ninazozijua ni Yanga, Simba na Azam”. “Na kuhusu Samatta ninamjua kwani nimeshamuona anavyocheza, ni mchezaji mzuri na ana maono mazuri kiuchezaji na kwamba akizidi kujituma atafika mbali. Pia alisema malengo yake ni kusaidia vijana wadogo kukuza vipaji vyao vya soka na kuwapa motisha za kimichezo ili wawe na moyo wa kuupenda mchezo huo. Nyota huyo wa Tottenham, anatarajiwa kutembelea vivutio mbalimbali vya kitalii ikiwa ni sehemu ya kupumzika kama wanavyofanya nyota mbalimbali barani Ulaya ambao wengi wao hukimbilia kisiwa cha Ibiza nchini Hispania.

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA