Yai kwa siku husaidia watoto wadogo kuongeza kimo


yai iliyochemshwaHaki miliki ya pichaDERKIEN/GETTY
Kula yai kwa siku kunaweza kuwasaidia watoto wadogo wenye utapiamlo kuongeza urefu kulingana na utafiti wa miezi sita huko Ecuador.
Haijalishi ikiwa ni yale yaliyo chemshwa, au ya kukaanga, na watafiti wanasema ni njia isiyo ghali ya kuzuia kudumaa.
Miaka miwili ya kwanza maishani ni ya muhimu sana kwa ukuaji na maendeleo na kudumaa kunaweza kuleta madhara makubwa.
Lishe duni ni sababu kubwa ya kudumaa, pamoja na maambukizi ya utotoni na magonjwa.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, watoto milioni 155 chini ya umri wa miaka mitano wamedumaa (wafupi kwa umri wao).
Wengi wao wanaishi katika nchi zilizo na mapato ya chini na ya kati na wataalamu wa afya wamekuwa wakitafuta njia za kukabiliana na suala hilo.
Lora Iannotti na wenzake walifanya majaribio katika nyanda za vijijini ya Ecuador na kuwapa watoto wadogo sana (wenye umri wa miezi sita hadi tisa) mayai, ili kuona kama yataweza kuwasaidia.
Nusu tu kati ya watoto 160 ambao walishiriki katika majaribio walilishwa yai kila siku kwa muda wa miezi sita - wengine walifuatiliwa tu kwa sababu za ulinganifu.
Kudumaa hakukuonekana sana miongoni mwa wale waliolishwa mayai baada ya majaribio kumalizika. Maambukizi yalikuwa ni asilimia 47 chini ya yale ambao hawakula yai.
Baadhi ya watoto katika kundi lile lingine walikula mayai lakini sio kila siku.
Mtafiti kuu Bi Iannotti alisema: "Sisi tulishangazwa na nafuu iliyoletwa na jaribio hili.
"Na ni vyema sana kuwa ni njia iliyo nafuu sana hasa kwa watu wanaishi katika mazingira magumu au walio na upungufu wa lishe."
Mayai yana mchanganyiko wa madini, ambayo ni muhimu," alisema.
WHO inapendekeza akina mama duniani kote wawanyonyeshe watoto wachanga kwa miezi sita ili wakuwe kikamilifu kiafya. Baada ya miezi sita ya kwanza, watoto wachanga wanafaa kupewa vyakula nyongeza na kuendelea kunyonyeshwa hadi umri wa miaka miwili au zaidi.
Shirika la lishe la Uingereza linshauri: "Licha ya kuwa mayai ni chakula bora, ni muhimu sana watoto wadogo wapate aina tofauti tofauti ya vyakula . Sio tu kwa ajili ya kupata vitamini na madini wanayohitaji, lakini pia kuwapa uzoefu wa ladha tofauti tofauti.
"Idadi kubwa ya vyakula vya protini inapaswa kutolewa kwa watoto wadogo,ikiwemo mayai, maharagwe,samaki,nyama na maziwa."
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

KWA HERI KAMANDA WETU ABBAS KANDORO

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.

YANGA SC WAANZA KAZI AFRIKA LEO…WANAKIPIGA NA U.S.M. ALGER SAA 4:00 USIKU ALGERIA

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA