YANGA SC: HATUSAJILI BENDERA FUATA UPEPO, TUNAFANYA MAMBO ‘KIPROFESHENO’


Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
YANGA SC imesema haisajili kwa bendera kufuata upepo, bali inazingatia mahitaji yake ndani ya kikosi kutokana na ripoti ya benchi la Ufundi.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa katika mahojiano maalum na Bin Zubeiry Sports – Online leo mjini Dar es Salaam.
“Tunafanya zoezi hili kwa mujibu wa ripoti ya mwalimu, hatutaki kusajili kwa sababu tumesikia timu nyingine zinasajili. Tunafanya mambo yetu kimya kimya na mwisho wa siku wapenzi na wanachama wa Yanga watafurahi na roho zao,”amesema Mkwasa.
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema tayari wamekwishamalizana na wachezaji watatu wapya 

Katibu huyo amesema Yanga ina maeneo madogo tu ya kubadilisha na haihitaji kubadilisha timu nzima kama zinavyofanya timu nyingine.
Pamoja na hayo, Mkwasa amesema tayari wamekwishamalizana na wachezaji watatu wapya, lakini kwa sasa wataendelea kufanya siri.
“Tumekwishasajii wachezaji watatu wapya tumewapa mikataba tena kwa maridhiano na klabu zao, sasa tunasaubiri muda ufike tuwatangaze,”amesema Mkwasa.
Mkwasa amesema hawataki kukurupuka kutangaza mchezaji kabla ya dirisha la usajili halijafunguliwa rasmi na wachezaji hao pia hawajamaliza kabisa mikataba na klabu zao, ili wasije kuadhibiwa tena.
“Sisi tunatakiwa kuwa makini kidogo, yasije yakatupata yaliyotupata kama ya Kessy (Hassan) kwa sababu tulipigwa faini Sh. Milioni 50 kwa kusajili mchezaji bado wiki moja tu amalize kabia mkataba wake,” amesema.
Mkwasa alikuwa anakumbushia usajili wa beki Hassan Kessy msimu uliopita kutoka kwa mahasimu, Simba SC ambao waliingia naye mkataba na kuanza kumtumia akiwa amebakiza wiki moja kumaliza kabisa mkataba wake na klabu yake ya zamani, hivyo mwisho wa siku Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) likawapiga faini ya Sh. Miliomi 50. 

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MAMEYA WA TEMEKE, UBUNGO WATWANGANA UCHAGUZI WA NAIBU MEYA DAR

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

RAIS MSTAAFU KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA MWANAHABARI ATHUMAN HAMISI DAR