4x4

YANGA YAIBUKA KIDEDEA DHIDI YA TUSKER YA KENYA

Yanga imeifunga Tusker ya Kenya penalti 4-2 katika mchezo wa Ligi ya SportPesa Super Cup kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam leo baada ya kutoka suluhu ndani ya dk 90.

Kwa ushindi huo Yanga imeingia nusu fainali ya Kombe hilo ambapo itapambana na FC Leopard ya Kenya ambayo imefuzu baada ya kuifunga Singida United kwa penalti 5-4 baada ya kutoka sare ya 1-1 katika kipindi cha dk 90..

Kipa wa Yanga, Deo Munishi maarufu kama Dida alichangia kung'olewa kwa Tusker baada ya kupangua moja ya mikwaju ya Wakenya hao.

Sasa Yanga itakutana na Wakenya wengine, safari hii ni AFC Leopards ambao wameing'oa Singida United kwa mikwaju ya penalti pia.

Post a Comment