3 of 3,202 Print all In new window MAONESHO YA SABASABA 2017: WENGI WAJIUNGA NA PSPF KUPITIA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI PSS


 Meneja wa mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi. Mwanjaa Sembe, (kulia), akimkabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko huo kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari, Mwanafunzi wa chuo cha Uhasibu (TIA), Bi.Demetriz Bayona, baada ya kujiunga na Mfuko huo leo Julai 2, 2017. Wananchi wengi waliotembelea banda la Mfuko huo leo, wamejiunga na mpango huo baada ya kupatiwa elimu na faida ambazo mwanachama anapata endapo atajiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari ambapo kujiunga hakuna masharti isipokuwa kwa mtu yeyote mwenye kazi ya kumuingizia kipato na atatakiwa kuchangia au kuweka akiba ya kima cha chini cha shilingi elfu 10 kila mwezi. Miongoni mwa faifa ambazo mwanachama aliyejiunga na mpango huo ni pamoja na kujipatia bima ya afya, itakayomuwezesha kupata matibabu yeye mwanachama na wategemezi wake watatu. Lakini pia kujipatia mafao mablimbali yakiwemo fao la elimu, lakini pia mkopo wa nyumba na viwanja kutegemea na akiba ambayo mwanachama amejiwekea.
 Wanachama wapya wa PSPF wakijaza fomu za kujiunga na mpango wa PSS
 Bi Amina Mtoo akijaza fomu za kujiunga na uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari, (PSS), leo Julai 2, 2017
 Mwanachuo wa chuo cha Uhasibu jijini Dar es Salaam, Bi.Demetria Bayona, akisikiliza kwa makini faida za kujiunga na PSPF kupitia  mpango wa PSS kutoka kwa afisa wa Mfuko huo. Baada ya kuelewa faida zake, Mwanachuo huyo hatimaye alijiunga na kupatiwa kadi yake ya uanachama ndani ya dakika 20.
 Menenja wa Mpango wa uchangiaji wa hiari, (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Mwanjaa Semba, (kulia), akitoa somo kwa mwananchi aliyetembelea banda la Mfuko huo kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam leo Julai 2, 2017
 Meneja Usimamizi wa na utawala wa mifumo ya TEHAMA, wa  Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Bernard Ntelya, (kushoto), akimpatia maelezo mwananchi huyu aliyetembelea banda la PSPF Julai 2, 2017
 Afisa kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii, (SSRA), (kulia), akifuatilia jinsi maafisa wa PSPF wanavyotoa huduma kwa wanachama na wananchi wanaotembela banda la Mfuko huo. SSRA imeweka maafisa wake kila banda la linalotoa huduma ya hifadhi ya Jamii ili kusikiliza malalamiko ya wanachama husika wa Mfuko hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio, (kushoto), akikaribishwa na Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Coletha Mnyamani alipotembelea banda hilo leo Julai 2, 2017.
 Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Isack Kimaro, (kulia), akimuhudumia mwananchi huyu aliyefika kupata huduma kwenye banda la Mfuko huo leo Julai 2, 2017.
 Afisa wa PSPF, (kushoto), akimuhudumia mwananchi huyu aliyefika kupata huduma za Mfuko huo
 Bw. Kimaro (kulia), akimsaidia kutambua michango yake mwanachama huyu aliyefika kwenye banda la PSPF
 Afisa uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF anayeshughulikia masuala ya uchangiaji wa hiari (PSS), Bi. Asmahan H. Haji, akiwajibika ipasavyo kwenye dawati lake
 Bi Asmahan (kulia), akimkabidhi kadi ya uanachama wa PSPF kupitia mpango wa PSS, Bi.Amina Mtoo, ambaye alisindikizwa na mchumba wake, Bw. Ayoub Issa, leo Julai 2, 2017
 Afisa Uhusiano wa PSPF, Bi. Coletha Mnyamani, (kulia), akimkabidhi kadi ya uanachama wa PSPF, Bi. Gloria P. Nyange, akiwa na mwanae wa miaka minne Winprecious Noel baada ya kujiunga na PSS.
 Bi Mnyamani akimkabidhi kadi na nyaraka mbalimbali zinazoelezea jinsi mwanachama huyu mpya Bw.Kamaga Salim Kilolo, aliyejiunga na mpango wa uchagiaji wa hiari PSS.
 Mwananchi akijaza fomu chini ya usaidizi wa Afisa uendeshaji msaidizi wa PSPF
 Bi Asmahan H. Haji, (kulia), akimkabidhi kadi ya uanachama wa PSPF, Bi.Sabah A. Dossa, baada ya kujiunga na mpango wa PSS.
 Kabla ya kujiunga na mpango wa PSS, Bi. Amina Mtoo, (wakwanza kushoto) na mchumba wake, Bw. Ayoub Issa, walipata fursa ya kupewa elimu ya kina juu ya kujiunga na mpango huo na faida ambazo mwanachama atapata ikiwemo bima ya afya ambayo itawahusu wawili hao na wategemezi wao wawili
Bi. Mnyamani akimuhudumia mstaafu

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI