AMBER LULU ADAIWA KUVUTISHWA UNGA!SIKU zote ubuyu wa Zanzibar unahitaji mate mengi ili uumungunye sawia na uzuri wake ni kwamba haukinaishi! Muuza sura (video queen) ambaye hivi karibuni jina lake limekua kwa kasi baada ya kujiingiza kwenye Bongo FlevaLulu Augen ‘Amber Lulu anadaiwa kuvutishwa madawa ya kulevya ‘unga’.

Kwa mujibu wa mtoa ubuyu kindakindaki, mtuhumiwa namba moja wa kumharibu Amber Lulu kwa kumuingiza kwenye janga hilo ni mwanamuziki David Genz ‘Young D’ ambaye anadaiwa kuishi naye maeneo ya Mwananyamala, Kinondoni jijini Dar.
JIUNGE NA MTOA UBUYU
Mtoa ubuyu wetu huyo ambaye ni mtu wa karibu wa mastaa hao alinyetisha kuwa, Amber Lulu alianza kuishi na Young D kitambo tangu amwagane na video Queen mwingine, Tunda Sebastian.

Ilisemekana kuwa, chanzo cha jamaa huyo kuhamia kwa Amber Lulu ni skendo hiyohiyo ya unga ambayo ilisababisha Tunda kutajwa kwenye ile listi ya mastaa wabwia unga iliyotolewa na mkuu wa mkoa miezi kadhaa iliyopita.
Madai mazito yalizidi kushushwa kwamba, mwanamuziki huyo alipohamishia majeshi kwa Amber Lulu ndipo akaanza kumfundisha bidada huyo naye kuvuta ‘mambo meupe’ mdogomdogo.

“Unajua Young D alivyotemana na Tunda, alianza uhusiano wa kimapenzi na Amber Lulu. Kama mtakumbuka, jamaa ndiye aliyetuhumiwa kumuingiza Tunda kwenye unga uliosababisha kukumbwa na ule msala wa kutajwa na kufikishwa polisi kwa sababu ya matumizi ya madawa ya kulevya.
“Unajua mara nyingi Young D yupo kwa Amber Lulu. Wanapika na kupakua na muda mwingi wakiwa ndani inasemekana huwa wanavuta unga.“Unaambiwa sasa hivi hata ukisikiliza sauti ya Amber Lulu siyo ile ya kawaida, imeharibika kwa sababu ya matumizi ya unga.
“Kiukweli ni ishu ambayo imetukera sana na tunamhurumia kwa sababu tunakwenda kumpoteza wakati ndiyo kwanza ameanza kula matunda ya sanaa yake maana anapata shoo lakini tunaamini hata hela atakayokuwa anapiga itaishia kwenye unga ilihali familia yake kule Mbeya inamtegemea,” alimaliza kutiririka mtoa ubuyu wetu akiomba wadau kufanya juu chini kumuokoa Amber Lulu na balaa hilo.

AMBER LULU ABANWA
Baada ya kumwagiwa ubuyu huo, kama ilivyo desturi ya Wikienda, lilisaga soli hadi nyumbani kwa Amber Lulu anakodaiwa kuishi na Young D, Mwananyamala-Garage lakini Young D hakuwepo.
Katika kumbana Amber Lulu ndipo akaridhia kufunguka juu ya sakata hilo ambapo mahojiano yalikuwa hivi;

Wikienda: Mambo vipi Amber Lulu? Nimekutafuta wiki nzima sikukupata…
Amber Lulu: Nilikuwa safarini, haya karibu.
Wikienda: Kuna madai kuwa hivi sasa umejitumbukiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya na aliyekuingiza ni Young D, je, jambo hili likoje?
Amber Lulu: Kivipi?

Wikienda: Ni kwamba kuna madai kuwa sasa hivi unaishi na Young D, mnapika na kupakua. Inasemekana Young D ndiye anayekuvutisha unga…
Amber Lulu: Mimi kwa sasa nimeachana na Young D na hakai hapa nyumbani kwangu. Au umemkuta hapa kwangu?
Wikienda: Hivyo ndivyo ubuyu unavyosema, je, ukweli ni upi?
Amber Lulu: Hapana, nilishaachana naye muda mrefu na hakai tena kwangu.
Wikienda: Hata kama hakai hapa nyumbani kwako, je, ni kweli ndiye amekufundisha kubwia unga?
Amber Lulu: Sivuti unga na ninaomba uniulize kuhusu wimbo wangu wa Watakoma unavyokimbiza kwa sasa.

NENO LA MHARIRI
Habari ya mjini kwa sasa ndiyo hiyo na ubuyu mtamu umeupata ila kama kweli Amber Lulu amejitumbukiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya, basi atakuwa anaharibu ndoto zake za kuwa mwanamuziki bora wa kike hapa Bongo.

Ubuyu: Imelda Mtema | IJUMAA WIKIENDA| Dar

Amber Lulu ni Noma Stejini… Cheki Alichokifanya Hapa

Stori zinazo husiana na ulizosoma

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

PADRI AUGUSTINO RAMADHANI AONGOZA IBADA YA KUMBUKUMBU YA MKE WA PROFESA SHABA DAR

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.