BUSWITA, AJIBU ‘WATEKA’ MASHABIKI MAZOEZINI

ChArity JAmes
BAADA ya mazoezi ya wiki mbili ya ‘gmy’, kikosi cha Yanga leo chini ya Kocha Mkuu, George Lwandamina kimetumia saa mbili kujifua katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam huku Ibrahim Ajibu akianza kuonesha makali yake. Mazoezi ya Yanga yalianza saa tatu asubuhi na kumalizika saa tano katika uwanja huo huku vikosi viwili vya timu hiyo vikioneshana uwezo kwa kuhakikisha kila mchezaji anaonesha makali yake na kujitengenezea nafasi ya kupata namba katika kikosi cha kwanza. Vikosi vilikuwa viwili ambapo kila kikosi kilipata bao mbili mbili ambapo katika kila kikosi kilitoa mfungaji mmoja ambaye ndiye aliyefunga bao zote mbili. Katika mazoezi hayo kiungo kutoka
Mbao FC, Pius Buswita alionesha makali zaidi baada ya kukwamisha bao mbili zilizoisaidia timu yake kuweza kutoka sare na kikosi cha pili cha timu hiyo. Wakati Buswita akionesha makali hayo, Ajibu naye hakutaka kubaki nyuma alitoa pasi nzuri ambayo ilizaa bao lililofungwa na Geofrey Mwashiuya ambaye ndiye aliyefunga mabao yote mawili katika kikosi hicho ambacho kilikuwa kinaundwa na washambuliaji nyota Amisi Tambwe na Obrey Chirwa. Si kutoa pasi tu lakini alionesha ana kitu kazi cha ziada kwa jinsi alivyokuwa akicheza na kushirikiana na wenzake. Akizungumza na gazeti hili mara baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo, Meneja wa klabu hiyo, Hafidh saleh, alisema kikosi sasa kitaendelea na mazoezi ya uwanjani baada ya kufanya mazoezi ya
gmy kwa muda wa wiki mbili. “Kama unavyoona mazoezi ya uwanjani yameanza leo na tunatarajia kuendelea nayo tena kesho jioni katika uwanja huu huu hadi hapo tutakapoondoka kwenda Morogoro kwaajili ya kambi ya muda kwaajili ya kujiweka sawa na mashindano yaliyo mbele yetu,” alisema. Saleh alisema kutokana na kufanya mazoezi kwa muda mrefu wameamua kuwapumzisha wachezaji wao kesho asubuhi na kuendelea na mazoezi hayo jioni katika uwanja huo. Alipoulizwa juu ya wachezaji wao kama wote wameweza kujiunga kikosini, alisema asilimia 90 ya wachezaji wao wote wameanza mazoezi na kwamba mshambuliaji wao wa kimataifa, Donald Ngoma anatarajia kuungana na wenzake katika mazoezi hayo ya jioni.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.