DC MTATURU ASHIRIKI MAZOEZI YA VIUNGO NA WANANCHI


Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akipiga danadana  kama moja ya mazoezi hayo.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akikabidhi mpira wa miguu kwa timu ya walimu ya wilaya hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akiwa katika picha ya pamoja na wananchi walioshiriki mazoezi hayo.
....................................................................................
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu leo asubuhi ameshiriki mazoezi ya viungo pamoja na  wananchi wa Kata ya Puma wilayani humo  lengo likiwa ni kuunga mkono maelekezo ya makamu wa Rais Samiah Suluhu Hassan ya kufanya mazoezi kila jumamosi ya pili ya kila mwezi.

Akiwa katika mazoezi hayo msisitizo wake mkubwa  kwa wananchi ni kujenga utaratibu wa kufanya mazoezi ili kuweza kuondokana na  magonjwa yasiyo ya kuambikiza na kuufanya mwili kuwa imara katika utendaji wao wa kazi.

Aidha amewataka kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara kwa kuwa uchumi wa Taifa unajengwa na wananchi walio na afya imara.

Mbali na kufanya  mazoezi hayo  amekabidhi mpira wa miguu kwa ajili ya timu ya walimu ya wilaya lengo likiwa ni kujenga ari kwa wananchi kupenda michezo na hivyo kuweza kuinua kiwango cha soka wilayani humo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*