DEGE LA KIVITA LASABABISHA MTAFARUKU DAR

Dege la kivita lililokuwa likifanya mazoezi katika anga la Dar es Salaam limesababisha mtafaruku mkubwa kwa wakazi jiji hilo.

Kitendo hicho kilitokea majira ya saa 3 asubuhi na kusababisha kila mmoja kuelezea kivyake kuhusu dege hilo lililokuwa na muungurumo mkubwa huku likiwa kwenye mwendo kasi na kimo cha chini.

"Mimi nilivyosikia muungurumo huo nilistuka na kuachia usukani na gari kupoteza mwelekeo kuelekea kwenye mtaro kabla ya kulizuia tena," alisema dereva huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja.

Mteja mmoja  aliyekuwa katika jengo kubwa la kibiashara la Quality Centre, Barabara ya Nyerere, alisema kuwa walikumbwa na hofu kiasi cha kufikiri kuwa dege hilo limetua ghafla kwenye jengo hilo, hali iliyosababisha watu wengi waliokuwemo huo kupatwa na viwewe wasijue la kufanya.

Baadhi walisikika kuwa huenda wanajeshi walikuwa wanaendelea na mazoezi ya kivita hasa ikizingatiwa kwamba jana  Julai 25,ilikuwa Siku ya Mashujaa ambayo hata hivyo haikusherehekewa kama ilivyo kawaida miaka mingi iliyopita.

Rais John Magufuli ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu akiwa mkoani Singida kwa ziara ya kikazi jana, aliwaomba wananchi kwenye mkutano wa hadhara kusimama kwa muda wa dakika moja kuwaombea dua wanajeshi wote walikufa vitani na kueleza kuwa  mwaka huu Siku ya Mashujaa haitakuwepo bali  itasherehekewa kwa wahusika  kushiriki kwenye shughuli za kijamii.

Sababu za Siku hiyo ya mashujaa kutoadhimishwa mwaka huu hazikuweza kutajwa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.