4x4

KARIA, MADADI WATEULIWA KUWARITHI MALINZI, MWESIGWA TFF


Wallace Karia (kushoto) na Salum Madadi.

KAMATI ya utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imemteua makamu wa rais wa shirikisho hilo, Wallace Karia kuchukua kwa muda nafasi ya rais wa shirikisho hilo, Jamal Malizi huku pia ikimteua Salum Madadi kuwa katibu mkuu wa shirikisho hilo.

Hatua hiyo imefikiwa leo hii katika mkutano maalumu wa kamati hiyo ulichofanyika Makao Makuu wa TFFjijini Dar es Salaam.

 

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema kuwa kamati hiyo ya utendaji ya TFF, imefika uamuzi huo kutokana na Malinzi pamoja na katibu mkuu wa shirikisho hilo Selestine Mwesigwa kushikiliwa na Taasisi ya Kupambana na Rusha Tanzania  (Takukuru) kwa  makosa mbalimbali likiwemo la utakasishaji fedha ambayo yaliwafanya juzi Alhamisi kufikishwa kwatika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kusomewa mashitaka.

“Kutokana na ha hiyo kwa kamati ya utendaji imeamua kuwateua viongozi hao kukaimu nafasi hizo ili kazi shirikisho ziweze kuendelea kama kawaida.

“Kwa hiyo kuanzia sasa Karia atakuwa Kaimu Rais wa TFF na Mdadi atakuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF,” alisema Lucas.
Post a Comment