MAZISHI YA MKONGWE WA MUZIKI, SHAABAN DEDE


Hali halisi nyumbani kwa marehemu

Mwimbaji mkongwe nchini wa muziki wa dansi, Shaban Dede aliyefariki dunia jana asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa siku kadhaa akitibiwa amezikwa leo katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Jeneza lenye mwili wa marehemu

Watu wamejaa nyumbani kwa Marehemu, Mtaa wa Congo/Kibambawe, Jaqngwani Karikaoo kwa ajili ya shughuli nzima ya kuaga na kuuzika mwili wa marehemu Dede.


Dede atakumbukwa kwa umahiri wa tungo zake za nyimbo kama vile Kilio Cha Mtu Mzima, Kaza Moyo (Msondo), Diana, Tui la Nazi, Amina (Sikinde), ambazo zinaonesha uhalisia wa maisha ya watu na zilijizolea umaarufu katika kumbi mbali mbali za muziki na kuvuta mashabiki wa rika zote.

Waombolezaji msibani.

Dede, alikuwa mwanamuziki mkubwa ambaye alikuwa akiitumikia Msondo Music Band lakini huko nyuma aling’ara na Bendi za Mlimani Park “Sikinde”, Bima Lee, alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya sukari pamoja na figo.

Mwili wa marehemu ukipelekwa makaburini kwa ajili ya mazishi.


 
Shughuli ya mazishi ikiendelea.
Na Richard Bukos | Global Publishers

Live; Mazishi ya Mkongwe wa Muziki, Shaaban Dede, Kisutu Dar

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*