4x4

MBUNGE HALIMA MDEE AFIKISHWA MAHAKAMANI

 Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee (kushoto) akisalimiana na Mbunge wa  Bunda Mjini, Esther Bulaya  akiwa amehifadhiwa katika ukumbi wa wazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu Dar es Salaam, akisubiri kusomewa kesi yake.
 Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Kushoto) akiwa chini ya ulinzi wa Askari katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana akisubiri kusomewa shitaka linalomkabili, Halima anatuhumiwa kwa kutoa lugha za matusi kwa Rais John Magufuli wakati akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni
 Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Katikati) akisalimiana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe katika Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana kabla ya kusomewa shitaka linalomkabili, Halima anatuhumiwa kwa kutoa lugha za matusi kwa Rais John Magufuli wakati akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni.
 Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (katikati) akiwashukuru wafuasi wa Chadema wakati akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana baada ya kuachiwa huru kwa dhamana. Halima anatuhumiwa kwa kutoa lugha za matusi kwa Rais John Magufuli wakati akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni.

Post a Comment