MCHEZAJI NGULI WA ZAMANI WA EVERTON OSMAN ATUA NCHINI, KWENDA KUTALII NGORONGORO CRATER

 Mchezaji Nguli wa zamani wa Everton ya Uingereza, Leon Osman akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam, kuhusu shughuli mbalimbali atakazozifanya nchini kabla ya timu ya Everton kuchuana na washindi wa Kombe la SportPesa, Gol Mahia ya Kenya Julai 13, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

Julai 10, atatembelea Mbuga ya Wanyama ya Ngorongoro Crater ili kujionea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini, lakini pia atapata nafasi ya kukutana na waandishi wa habari na wachambuzi wa soka nchini katika semina ya kuwajengea uwezo itakayofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Julai 12. mwaka huu. Ratiba hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Utawala  na Utekelezaji wa SportPesa, Tarimba Abbas.

Leono Osman alieleza jinsi alivyo na shauku kubwa ya kutembelea vivutio mbalimbali vya Tanzania  huku akielezea jinsi ujio wa Everton utakavyoinufaisha Tanzania.(PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

 Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Geofrey Meena (wa pili kushoto) akizungumza katika mkutano huo ambapoalitoa offer kwa Leon Osman kuetembelea Ngorongoro Crater.
Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Tarimba Abbas akielezea ratiba ya Leon Osman na ujio wa timu ya Everton nchini.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA