MR NICE AFANYIWA KITU MBAYA GESTI


Mr. Nice kwenye varangati hilo.
DAR ES SALAAM: Mfalme wa Takeu, Lucas Mkenda maarufu kama Mr. Nice juzi Jumatatu alifanyiwa kitu mbaya mae­neo ya uswahilini, Manzese Uwanja wa Fisi jijini Dar baa­da ya kuwa amelewa, Risasi Mchanganyiko lina mkanda kamili.
MWANZO WA MCHEZO HUU HAPA
Baadhi ya mashabiki wa Muziki wa Dansi waliliambia Risasi Mchanganyiko kuwa walimuona Mr. Nice usiku akiwa katika ukumbi mmoja wa starehe uliopo Kinondoni, ambako Bendi ya Muziki ya Mapacha Watatu ilikuwa iki­tumbuiza.
Mmoja wa wakurugenzi wa bendi hiyo, ambaye pia ni mwimbaji nyota, Jose Mara inasemekana alimuita juu ya jukwaa Mr Nice na kumtaka kuwasalimia mashabiki wake ambao wamem-miss kwa muda mrefu.
APANDA JUKWAANI, MMMH!
Chanzo chetu kilichokuwa ndani ya ukumbi huo, kinase­ma mkali huyo wa muziki, aliitika wito na kupanda juk­waani, lakini katika kuwasal­imia mashabiki, inadaiwa kidogo ilikuwa ni shida kwa kuwa alikuwa ameburudika vya kutosha.

Varangati likiendelea.

AONDOKA USIKU MNENE NA ‘MZIGO’
Chanzo chetu kinaeleza kuwa baada ya kuburudika vya kutosha katika ukumbi huo, usiku mnene, Mr Nice ambaye inadaiwa hali yake ya kifedha imeanza kurejea kuwa nzuri, aliondoka akiwa ameambatana na msichana ambaye jina lake halikufa­hamika mara moja.
Safari yake na mwanamke huyo, iliwafikisha katika ny­umba moja ya kulala wageni iliyopo Uwanja wa Fisi, Man­zese ambako walichukua chumba na kuingia ndani.
SAA TANO ASUBUHI
Shuhuda wetu aliyekuwa miongoni mwa watu wal­iokuwepo eneo la baa hiyo, anadai ilipofika saa tano as­ubuhi, Mr Nice aliamka, lakini mwanamke aliyekuwa naye hakuwepo.
Hali hiyo ilimpa wasiwasi msanii huyo, aliyeanza ku­jisachi na kugundua kuwa kiasi cha shilingi 230,000 hakikuwepo mfukoni mwake, ikiwa ni pamoja na simu yake aina ya Apple na mazagaza­ga mengine kadhaa.
AANGUA KILIO, AJAZA WATU
Bila kujali ustaa wake, in­adaiwa Mr Nice aliangua kilio kikubwa kilichosababisha watu kujaa ili wajue kulikoni.
Msanii huyo mwenye re­kodi ya kuwahi kushika pesa nyingi kupitia muziki, ali­waeleza watu kilichomsibu hivyo kuwaomba vijana wa­naomfahamu msichana ali­yekuwa naye, wamtafute kwa udi na uvumba na kuwaahidi kama wangempata, angewa­pa kitu kidogo.

Mr. Nice kwenye hekaheka.

DEMU ASAKWA, AIBULIWA
Vijana wa maeneo hayo ambao wanamfahamu msichana huyo, walimtaja kuwa ni Happy baada ya ku­pewa tenda hiyo, walianza kumsaka kwa bidii na kufani­kiwa kumnasa muda mch­ache baadaye ambako wal­impeleka kwa mkali huyo wa muziki aliyetamba sana enzi zake.
MR NICE ALIANZISHA, POLISI WAITWA
Baada ya msichana huyo kuletwa mbele ya Mr Nice akiwa na simu aliyoondoka nayo, msanii huyo alianzi­sha vurugu kubwa kwa dada huyo, kiasi cha kuwapa hofu baadhi ya watu, ambao wali­wapigia simu polisi waliowa­sili muda mchache baadaye na kuweza kutuliza hali ya hewa.
Wanausalama hao wal­ipofika eneo hilo walimtaiti Mr Nice ambaye wakati huo alionekana kuwa bado amechangamka.
Kuona hivyo, polisi wal­imchukua na msichana huyo pamoja na watu wengine kadhaa waliokutwa wakiwa wanapata ‘kiburudisho’ nda­ni ya gesti hiyo na kwenda nao Kituo Kidogo cha Polisi Tandale ambako walifunguli­wa jalada la kunywa pombe wakati wa muda wa kazi.

Wananchi wakitaharuki.

ANG’ANG’ANIWA, DEMU AACHIWA
Mwanamuziki huyo ak­iwa kituoni hapo, al­ianza kulia kwa sauti na kuwaomba askari wamsamehe, huku aki­sisitiza kuwa yeye ame­shamsamehe msichana aliyemuibia fedha zake kwa kuwa shida yake kubwa ilikuwa ni kupata simu yake.
Licha kusema am­emsamehe mwa­namke huyo, lakini walimng’ang’ania kwa kosa la kunywa pombe asubuhi. Happy alia­chiwa na polisi baada ya kujitetea kuwa ali­ichukua simu hiyo kwa kuwa ni ya mpenzi wake na hakuwa na nia ya kuiiba isipokuwa alitoka kidogo kwenda kununua dawa, kitu kilichomfan­ya mpenzi wake huyo aamini aliachwa kwenye mataa.
AHAMISHIWA MAGOMENI
Risasi Mchanganyiko ambalo lilifika kituoni hapo na kumshuhu­dia msanii huyo akiwa ndani ya kituo, lilimuo­na akiondolewa kituoni hapo huku baadhi ya askari wakidokeza kuwa alipelekwa Kituo cha Polisi Magomeni.
Mr Nice ni msanii aliyetamba vilivyo ka­tika miaka ya mwan­zoni mwa 2000, akiimba vibao kama Kikulacho, Rafiki, Kidali Poo, Fagil­ia, King’asti na nyingine kadhaa.
RICHARD BUKOS, RISASI MCHANGANYIKO

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA