4x4

MSHAHARA MPYA WA LIONEL MESSI KUFURU TUPUMshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi.
LIONEL Messi amesaini mkataba mpya unaomfanya alipwe mshahara ambao umevuka kiwango kinachotakiwa kulipwa kwa mchezaji, lakini Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu, amesisitiza fowadi huyo anastahili alipwe hivyo kwa kuwa ni mchezaji bora zaidi katika historia ya soka.
Messi, analipwa pauni 500,000 (Sh bilioni 1.4) kwa wiki, katika mkataba wa miaka minne unaotarajiwa kumalizika mwaka 2021.
Rais huyo amepuuza uvumi kwamba mshahara huo unaweza kuwaletea matatizo Barcelona kutoka kwa Shirikisho la Soka Ulaya, kupitia kitengo chao cha Financial Fair Play.
Post a Comment