POLISI WAMTIA MBARONI HALIMA MDEE, APELEKWA KITUONI OYSTERBAY



Mbunge wa Kawe, Halima Mdee  (Chadema) jana jioni alikamatwa na Jeshi la Polisi akiwa nyumbani kwakeMakongo Juu jijini Dar es Salaam kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Alli Hapi na kupelekwa katika Kituoni cha Polisi Oysterbay.
Katibu wa CHADEMA jijini Dar, Henry Kilewo amethibitisha kukamatwa kwa Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA).
“Ni kweli Halima amekamatwa na Polisi na kupelekwa kituoni Oysterbay, alisema Kiwelo.
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Suzan Kaganda amesema amefanya hivyo kwa amri ya mkuu huyo wa wilaya.


“Wapi kakamatwa? Sisi tunachojua ni kuwa tunatekeleza agizo la DC (mkuu wa wilaya) mengine muulize kamishna wa kanda maalum, nimetimiza,” alisema Kaganda.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi jana aliliagiza Jeshi la Polisi kumkamata na kumweka ndani Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima James Mdee kwa madai kuwa kauli yake aliyoitoa juzi, Jumatatu wakati akiongea na wanahabari ni ya uchochezi na ya kumfedhehesha Rais John Magufuli.
Ujumbe wa Halima Mdee Baada ya kukamatwa
“Wamekuja polisi kunichukua home! As we speak naelekea kituo cha polisi, probably Oysterbay au Central. Wasaidizi wangu watakuwa na taarifa zaidi za ninakoelekea!”

ZAIDI SOMA HAPA==>DC Kinondoni Aagiza Mdee Awekwe Ndani

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

𝙂𝘼𝙈𝙊𝙉𝘿𝙄 𝙆𝘼𝘾𝙃𝙀𝙕𝘼 𝙆𝙄𝘽𝙄𝙉𝙂𝙒𝘼.