SETHI AUGUA, KESI YAKE NA RUGEMALIRA YAAHIRISHWA


James Rugemalira(mwenye mvi) na mwenzake Harbinder  Singh Sethi wakifikishwa mahakani leo.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeahirisha kesi inayowakabili mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder  Singh Sethi na  mfanyabiashara James Rugemalira wanaokabiliwa na mashtaka 12, yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababisha serikali hasara.

Rugemalira na Harbinder Singh Sethi baada ya kutoka kortini.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 22, mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi MkuuHuruma Shaidi baada ya wakili wa serikali, Leornad Swai, kueleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Mawakili wanaomtetea mfanyabiashara Harbinder Singh Sethi wameiomba Mahakama imruhusu mteja wao akatibiwe nje ya nchi, kutokana na kuwa na uvimbe na Baloon tumboni hali inayomsababishia maumivu makali na kumnyima usingizi kwa wiki ya nne sasa, ombi ambalo limekataliwa na Mahakama na kuagiza atibiwe Muhimbili.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI